Katika hali inayoonyesha umasikini mkali unalikabili taifa,Mwenyekiti wa Kijiji huko Chalinze alikutana na Waziri January Makamba hali ya kuwa shati lake limechanikachanika
Mwenyekiti huyo aliyesifiwa na Waziri Makamba kuwa ni mtunza mazingira mzuri,aligusa imani NA huruma ya Waziri January Makamba ambaye alilazimika kumpa shati lake,kitendo kilichomfanya Mwenyekiti huyo wa Kijiji aangue kilio kikuu
TAFSIRI YANGU
Hali ya umasikini ni mbaya sana mitaanj,mtu mzima kutembea amevaa shati
lililochanika,tena yeye akiliona ni shati maalum la kumpokelea Waziri
aliye katika Ofisi ya Makamu wa Rais inasikitisha
Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani imekuwa ikitamba
kwamba ni serikali ya watu masikini,je hii inamaanisha kwamba
haitauondoa umasikini kwa kuwa ukiondoka basi inakosa mizizi?
Kilio cha Mwenyekiti huyo wa kijiji,mtu mzima,akatoa machozi baada ya kupewa shati nadhani ana mengi
katika familia yake,hatujui watoto wake wanavaa kweli? Wanakula? He hali
hii iko kwa watu wangapi katika utawala huu? Je naye ni mpiga dili?
Tangu serikali iingie madarakani hakuna program yeyote ya kuondoa
umasikini vijijini,matokeo ndio haya,NA utawala huu sasa una miaka
miwili NA nusu,bado miaka miwili uondoke
Pia kuna tamko la kuzuia mitumba eti tutakuwa tunapeleka sisi mitumba ulaya,kwa hali hii kweli?
Japo serikali hii anasema ni ya masikini,lakini haitakiwi kuzidisha idadi ya watu
masikini
Taifa likihoji kuhusu umasikini mkali ulioletwa NA awamu hii,jibu ni MLIZOEA DILI
Badala ya kusisimua uchumi,hela zote tumeficha Benki
Kuu,zilizobaki,tunawapeleka vijana wa kizungu wenye viwanda vya ndege za
bombadia NA dreamliner
Home
/
Uncategories
/
MWENYEKITI WA KIJIJI CHALINZE APEWA SHATI NA MHE. J MAKAMBA BAADA YA KUMWONA AMEVAA SHATI LILILOCHANIKA ISHARA YA UMASKINI ULIOKITHIRI
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Tusiongee mambo bila kuwa na utafiti wa kutosha juu ya yale tunayoongea. Unao uhakika gani kwamba watu wote wa vijijini hawana nguo za kuvaa? Una uhakika gani kwamba umaskini wake unaletwa na serikali au kutowajibika? Je katika kijiji hicho wangapibwaligawiwa mashati?
JibuFutaMtoa nada atuambie ni nchi gani duniani ambayo hakuna kabisa maskini hata kama sio kwa kiwango Chetu lakini kila nchi inao maskini kulingana na kiwango cha uchumi wake.
Nchi inajenga nguvu za kiuchumi sasa. Unataka ghafla maisha ya watu wake yawe kama ya wamarekani? Tuache lawama zisizo na kichwa wala miguu. Marais waliopita mliwasema maneno mengi juu ya kufufua uchumi, haya huyu amekuja na mpango wa kufufua uchumi ambao hata kipofu anaona kule tunakoelekea maneno tena. Mnataka serikali itakayofanyaje? Mnataka watu wagawiwe fedha bila kufanya kazi? Acheni maneno bana fanyeni kazi. Tusihukumu serikali Ä·wa kesi moja au mbili na kuona yale mengi mazuri yanayofanywa na serikali hii. Serikali haiwezi kupita kila nyumba ikigawa fedha au nguo lakini fursa zilizopo ndizo zinazotakiwa kutumika kujibu haja tulizo nazo.