Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MAAJABU: JIONEE MAENEO SABA YENYE ULINZI WA KUTISHA DUNIA

Kwa kawaida tunadhani kuwa sehemu ambazo zinapewa ulinzi mkubwa katika nchi yoyote ni Magereza, Ikulu na Benki ingawa zipo sehemu nyingine ambazo zinalindwa sana duniani.


Zifuatazo ni sehemu saba ambazo zinalindwa zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani.

1: Benki ya Federal Reserve

Hii ni Benki ambapo katika jiji la New York, Marekani ambayo inatumika kuhifadhi zaidi ya 25% ya dhahabu zote duniani. Benki hii ni moja kati ya sehemu zenye ulinzi mkali zaidi duniani ikiwa imejengwa kwa urefu wa futi hamisini kutoka usawa wa Bahari na inalindwa na zaidi ya wanajeshi 5,000.
IMG_9453.JPG
2: Jumba la Greenbrier

Jumba hili linapatikana katika mji wa Virginia, Marekani ambapo unaambiwa linatumika kuhifadhi vifaa vya nyuklia vya Marekani. Unaambiwa katika jumba hili ndipo viongozi wa juu wa serikali na kijeshi hufanyia mkutano na kuamua wapi watashambulia.
IMG_9454.JPG
3: Mpaka wa Korea Kusini na Korea Kaskazini

Huu ni mpaka ambao unazitenganisha nchi mbili mahasimu duniani. Ni moja kati ya sehemu ambazo zinalindwa zaidi duniani ambapo kuna zaidi ya wanajeshi 2,000 ambao hufanya doria a ulinzi. Ni vigumu kwa mtu kufika kwenye mpaka huu kwa sababu kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yako.
IMG_9455.JPG
4: Inapohidhiwa mitambo ya WikiLeakes

Miongoni mwa sehemu zinazopewa ulinzi mkubwa duniani ni pamoja na mahali panapohifadhiwa mitambo ya kundi la wanahabari wachunguzi ambao hutoa siri za nchi mbalimbali duniani wakiwemo viongozi wakubwa wanaotenda kinyume na taratibu za kiuongozi ikiwa ni pamoja na rushwa na matumizi mabaya ya ofisi. Mitambo hii ipo katika milima ya Sweden ambapo unaambiwa ina uwezo wa kuzuia mabomu ya nyuklia.
IMG_9456.JPG
5: Ghala la Doomsday

Ghala la Doomsday lipo katika Kisiwa cha Spitsbergen, Norway ikiwa ni moja kati ya sehemu zinazopewa ulinzi wa hali ya juu zaidi duniani. Ulinzi unaopewa ghala hili ni kwa sababu ndimo zilimohifadhiwa zaidi ya aina 3,000 za mbegu. Hii ni kulinda dunia iwapo kutatokea vita au majanga ya asili yatayakayosababisha uhaba wa duniani.
IMG_9457.JPG

6: Area 51

Hii ni moja kati ya sehemu zenye ulinzi mkali zaidi duniani. Ni eneo ambalo hutumika kutengeneza ndege za kivita za Marekani, mabomu ya nyuklia na vifaa vya kiteknolojia vilivyotumika katika safari ya mwezini mwaka 1945.
IMG_9458.JPG
7: Mlima wa Chuma

Mlima huu upo Pennsylvania, Marekani ambao unatumika kuhifadhi mitambo inayoendesha mitandao ‘internet’. Sehemu hii pia hutumika kuhifadhi data na nyaraka za siri za serikali ya Marekani.
IMG_9459.JPG
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni