=======UPDATES.
Tumefanikiwa kupata ndege aina ya DC 8 kutoka Shirika la Samaritan Purse linaongozwa na mtoto wa Billy Grahm, aitwaye Franklin Grahm kwa ajili ya kuwasafirisha watoto Doreen, Sadia, na Wilson pamoja na wazazi wao watatu (Mama zao), ikiwa ni pamoja na Muuguzi Simphorosa Silalye, na Daktari Elias Mashalla wa Mt Meru hospitali. Ndege hii inaondoka jioni ya leo kutoka mji Mkuu Charlotte, Jimbo la North Carolina nchini Marekani na inatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Kilimanjaro majira ya jioni, Jumamosi, Mei 13. Endapo upatikanaji wa visas utafanikiwa hapo kesho kama tunavyo tarajia, wasafiri wataondoka asubuhi ya Jumapili, Mei 14 kuelekea Amerika. Ndege hii aina ya DC 8 itatarajiwa kutua Mjini Charlotte, NC, na wagonjwa pamoja na waliowasindikiza wataingia katika ndege nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa (Air Ambulance) hadi mji wa Sioux City, Iowa ambako watapokelewa na Uongozi wa Hospitali na Mercy na Shirika la STEMM.
0 maoni :
Chapisha Maoni