Wenger: Sio rahisi kuwa katika timu nne bora Uingereza
Mkufunzi
wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kushindwa kwa timu yake kufanya
vizuri msimu huu kunamaanisha kwamba sio rahisi kwa timu kuwa katika
orodha ya timu nne bora msimu huu.
Raia huyo wa Ufaransa ameongoza The Gunners katika nafasi nne bora katika kombe la vilabu bingwa kwa miaka 20 iliopita.Lakini ikiwa imesalia mechi 10, Arsenal iko katika nafasi ya sita ikiwa ni nyuma ya timu nne zinaozoongoza ligi hiyo.
''Ni changamoto kubwa kuwa katika nafasi nne bora lakini nadhani inawezekana'', alisema Wenger.
''Nimeweza kufanikiwa kwa miaka 20 iliopita na ilikuwa vigumu. Sasa imekuwa muhimu so nafurahia kwamba watu wamegundua sio rahisi kama inavyoonekana''.
Mwaka 2012 Wenger alisema kuwa miongoni mwa nafasi nne bora ni sawa na kushinda taji na maoni hayo yaliungwa mkono na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola.
''Unapomsikiza Guardiola, alisema siku nyengine kwamba kumaliza miongoni mwa nafasi nne bora katika ligi ya Uingereza ni sawa na kushinda taji kwa sababu ni vigumu sana'',aliongezea.
0 maoni :
Chapisha Maoni