Picha: moja wapo ya vituo vya mafuta ambavyo kuanzia kesho wananchi wanatarajiwa kumiminika kwa wingi kujipatia huduma kufuatia EWURA kushusha bei kikomo kuanzia.
Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura)imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoaanza kutumika kuanzia kesho.Meneja wa Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka kwa Sh 3 itakuwa inauzwa Sh 2057 kutoka 2060, dizeli imepanda kwa Sh 12, kutoka Sh 1913 hadi 1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka 1952.
Kiguo alisema mabadiliko hayo ya bei yametokana na bei za mafuta katika soko la dunia kubadilika sanjari na mfuko wa bei na gharama za usafirishaji.
Source: mwandishi maalum - Tanzania Mpya Matukio
0 maoni :
Chapisha Maoni