Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

VIDEO YA KIKWETE AKISHUHUDIA KUAPISHWA MKEWE

Wakati mheshimiwa spika akitambulisha bungeni mheshimiwa Jakaya Kikwete rais wa awamu ya nne, yamelipuka makofi yaliyodumu kwa dakika kadhaa. Kama kawaida ya JK tabasamu lake halizeeki, bashasha ya uso wake haipotei licha ya umri kuzidi kusogea kwa kasi. Nadhani ndani ya moyo wake anawasanifu sana wale waliomwita yeye kuwa ni rais dhaifu. Hao hao wamelazimika kumsafisha kwa kumpa heshima ya standing ovation!. Hakuna rais wa Afrika ambaye anaweza kupata bahati ya kukutana na mizani iliyo sawa ya utoaji wa maoni wakati akiwa bado yupo Ikulu. Wakenya wanamdhihaki sana Uhuru Kenyatta lakini mambo anayoyafanya kwenye miundo mbinu ni makubwa sana, akitoka ikulu ataanza kukumbukwa na hawa wanaomsimanga leo hii. Naamini JK anao uwezo wa kuandika kitabu kutokana tu na tukio alilolishuhudia bungeni akiwa amekaa kwenye sehemu ya wageni waalikwa. Ni jambo lililochukua muda mfupi tu lakini wenye fikra zinazojiuliza maswali mengi wanaweza kupata maandishi ya kitabu cha kurasa hamsini na kuendelea. Hizi ndizo siasa za kiafrika, ambazo labda zipo hivi kwa sababu ya watu kutokuwa na elimu ya masuala mengi ya kiuongozi. Au hali ipo hivi kwa sababu tu ya vita za chini kwa chini ambazo ni za kimakundi. Kula maisha mzee Jakaya Kikwete, ila fanyia kazi la kuandika uzoefu wako mkubwa kwenye siasa haswa za ndani ya nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni