VODACOM WAONGEZA MDA WA MANUNUZI YA HISA KUWAPA WANANCHI WENGI FURSA !!
Vodacom Tanzania PLC tumeongeza muda wa zoezi la kuuza hisa za awali.
“Kuongezeka kwa muda wa kununua hisa utawawezesha watanzania wengi na taasisi mbalimbali zilizoomba muda uongezwe kushiriki kikamilifu katika mchakato huu mpaka mnamo tarehe 11, Mwezi Mei, 2017.”
“Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa watanzania ambao wamekwishajitokeza kuwekeza kwa kununua hisa zetu na tunawakaribisha ambao bado hawajanunua waweze kuchangamkia fursa hii katika kipindi cha muda huu mfupi wa nyongeza.” Alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC,Rosalynn Mworia #VodacomIPO #WekezanaVoda
0 maoni :
Chapisha Maoni