TANZIA: AHMED KATHRADA HATUNAYE
Mpinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ya enzi hizo, AHMED
KATHRADA amefariki dunia leo, akiwa hospitali jijini Johannesburg. AHMED
Mohamed KATHRADA, rafiki mkubwa wa hayati Mandela, alikaa jela kwa
miaka 26, 18 ikiwa katika gereza la Kisiwa cha Roben, jela nyingine
aliowahi kutumikia kifungo kitambo hiyo ni Pollsmoor (Pozamoyo) Jijini Cape Town.
AHMED KATHRADA alihukumiwa jela sambamba na Nelson Mandela katika kesi ya kupindua nchi enzi za Utawala wa
Makaburu, katika kesi hiyo walikuwa Jumla ya watu 8, baadhi ni Elias
Motsoaledi , Walter Sisulu, Mhlaba, Mlangeni, Govan Mbeki (Baba wa Thabo
Mbeki) na Denis Goldberg. Kathrada alitoka jela mwaka 1990, akiwa jela
alikuwa anatumia namba ya Mfungwa Na. 468/64.
AHMED KATHRADA alizaliwa mwaka 1929, alipozaliwa panajulikana kama
Schweizer Reneke, Transvaal, wazazi wake wote wawili walikuwa na asili
ya India. Ni mwana-ANC, mpambanaji na aliwahi kuwa Mbunge. Nchini Afrika
Kusina, AHMED KATHRADA ni maarufu sana kama Uncle Kathy.
Akiwa jela, jamaa alisoma university degrees zipatazo 4, BA (in History
and Criminology), B Bibliography (in African Politics and Library
Science), BA Honours (History) na BA Honours (African Politics). Mwaka
1994 Kathrada alichaguliwa kuwa Mbunge na pia akateuliwa kuwa Mandela's
Parliamentary Counsellor. Aliwahi kutunukiwa tuzo kubwa kuliko zote
katika ANC ijulikanayo kama “Isithwalandwe”.
Kwa walioangalia Tv wakati ule wa Msiba wa Mandela, hususani siku ya
Mazishi, AHMED KATHRADA alitoa speech moja iliokuwa na hisia kali sana
na ndiye yeye katika kuuelezea msiba wa Mandela alisema: “I have lost a brother!”
RIP AHMED KATHRADA.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni