Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

PROF. LIPUMBA AMEKUWA TAPELI WA KISIASA



Prof. Ibrahim Haruna Lipumba sasa amekuwa tapeli wa kisiasa. Anatumia njia na mbinu za matapeli wa aina nyingine katika kufanikisha mambo yake.

          Image result for lipumba images
Njia kuu ni kutaka kuaminika na kuungwa mkono na ambao 'wapo naye' lakini wanajifanya 'hawapo naye'. Prof. Lipumba analenga kumtapeli Msajili wa Vyama vya Siasa hapa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Prof. Lipumba anajua kuwa yeye na hata upande wake hauna mamlaka ya kumvua Ukatibu Mkuu Maalim Seif. Anajua fika kuwa kuna shauri liko Mahakama Kuu linalohusiana na mgogoro wa CUF. Anajua fika kuwa hata Uenyekiti wake wa CUF una utata kwakuwa naye 'alishafukuzwa' Uenyekiti na uanachama. Hata Magdalena Sakaya naye alishafukuzwa.

Prof. Lipumba anataka kumuaminisha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa CUF imefanya maamuzi na mabadiliko ya uongozi. Anataka kumuaminisha jaji Mutungi kuwa sasa signatories wa ruzuku za CUF ni yeye na Magdalena Sakaya. Huu ni utapeli wa wazi ambao Msajili wa vyama vya siasa anapaswa kuwa nao macho.

Upande wa Prof. Lipumba ulikuwa ukikwama kupata ruzuku kutokana na idhinisho la Katibu Mkuu wa CUF, kama mmoja wa signatories/watia sahihi wa kutoa pesa, kukosekana. Prof. Lipumba anadhani na kuamini kuwa kumpa cheo cha Katibu Mkuu Sakaya ni kupata watia sahihi. Anajidanganya. Maalim anapaswa kujitoa rasmi na Sakaya kuingia. Prof. Lipumba atakwama.

Wote wanaomuunga mkono Prof. Lipumba katika utapeli wake huu, kupitia mgongo wa siasa, hawalitakii mema Taifa hili na demokrasia yake. Kama mpenda demokrasia ya kweli, amani, uhuru na umoja wa Taifa, nitawaanika wote walio nyuma ya Prof. Lipumba katika jambo hili la maigizo na utapeli wa kujifanya anaweza kufanya atakalo CUF.

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Source: Jamii Forum
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni