Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MESSI ASIMAMISHWA MECHI 4



Messi apigwa marufuku mechi nne kwa kumtukana mwamuzi

Lionel Messi
Messi alionekana kukerwa na uamuzi wa kumwadhibu dakika za mwisho za mechi dhidi ya Chile

Nyota wa Argentina Lionel Messi amepigwa marufuku mechi nne za kimataifa kwa kumtukana mwamuzi msaidizi wakati wa mechi kati ya taifa lake na Chile siku ya Alhamisi mjini Buenos Aires.
Shirikisho la soka duniani FIFA, lilitangaza uamuzi huo saa chache kabla ya Argentina kukutana na Bolivia katika mechi muhimu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.
Argentina, walionekana kumkosa sana mshambuliaji huyo wa Barcelona, na walilazwa 2-0 katika mechi hiyo iliyochezewa mji wa La Paz.
Mabao ya Bolivia yalifungwa na Juan Carlos Arce na Marcelo Martins.

Source: Swahili BBC

 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni