Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) umeazimia kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kudai mambo 7 yanayohusiana na haki za binadamu ikiwemo sakata la matangazo mubashara ya vikao vya bunge (Bunge LIVE)
Kikao cha Bunge la Tanzania
Akitoa taarifa hiyo ambayo ni yaazimio ya mkutano wa wa siku mbili uliohusisha watetezi wa haki za binadamu, wadau pamoja na asasi mbalimbali za kiraia Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mtandao huo bwana Onesmo Ole Ngurumwa amesema kesi hizo zitafunguliwa hivi karibuni.
Ameyataja mambo mengine ambayo wameazimia kuyafikisha katika mahakama hiyo kuwa ni kupinga sheria ya huduma za habari iliyopitishwa hivi karibuni pamoja na suala la uchaguzi wa Zanzibar.
"Kuna wenzetu kutoka Zanzibar wamekuja na hoja ya uchaguzi wa Zanzibar, tumewasikiliza tukaona wana hoja, kwahiyo nalo tumelipitisha na tutalifiksha katika mahakama hiyo"
Onesmo Olengurumwa - Mkurugenzi THRDC
Jambo lingine litakalofikishwa katika mahakama hiyo ni migogoro ya ardhi hususani mgogoro wa Loliondo, na lingine ni kuiomba mahakama iwaamuru mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka na kutekeleza mkataba wa haki za binadamu kama ilivyo kwenye makubaliano ya kuundwa kwa jumuiya.
Amesema watetezi hao wamefikia maamuzi ya kuyapeleka kwenye ngazi hiyo ya mahakama baada ya kushindwa kupata haki katika mahakama za ndani ya Tanzania
Chanzo: IPP Media
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni :
Chapisha Maoni