Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

POLISI AUAWA DAR

Dar es Salaam. Ofisa wa Polisi ameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyerezi Kanga wilayani Ilala.
[​IMG]
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni

Taarifa zilizotufikia punde na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni zinasema aliuawa nyumbani kwake. Hata hivyo hakumtaja jina lake.

Taarifa zaidi zimesema ofisa huyo wa Polisi alikuwa akifanya kazi wilaya ya Kibaha na alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma hivi karibuni.

Kamanda Hamduni amesema taarifa zaidi kuhusu polisi huyo zitatolewa baadaye.

“Ni kweli kuna ofisa wa Polisi ameuawa niko eneo la tukio naomba mniache nifanye kazi tutawapa taarifa baadaye,” alisema.

Chanzo: Muungwana Blog
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni