Msemaji wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kiongozi huyo huwa anapumzisha macho tu na si kulala wakati wa mikutano kama wanavyoamini watu wengi.
"Rais huwa anasumbuliwa na mwanga mkali," George Charamba amenukuliwa akisema na gazeti la serikali la Herald.
Rais huyo kwa sasa yupo nchini Singapore akipokea matibabu maalum kwenye macho yake.
Bw Mugabe, 93, anapanga kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.
"Huwa najihisi kama mtu ambaye amekosa kutekeleza kazi yake vyema ninaposoma (kwenye vyombo vya habari na mtandaoni) kwamba rais alikuwa anasinzia katika makongamano - la hasha," Bw Charamba amesema.
Alilinganisha tatizo la Bw Mugabe na matatizo ya macho ambayo yalikuwa yanamsibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Bw Mandela alikuwa anatatizwa na mwanga mkali na wapiga picha hawakuruhusiwa kutumia mwanga wa kamera wakati wanapiga picha katika hafla zake.
Matatizo ya Bw Mandela yalitokana na kufanya kazi kwa muda mrefu katika timbo na pia kufungwa jela muda mrefu Robben Island.
Safari za Bw Mugabe za mara kwa mara nje ya nchi zimekuwa zikishutumiwa sana na wakosoaji wake.
Sekta ya afya nchini Zimbabwe imedorora na wahudumu wa afya hulalamika kwamba huwa hawalipwi vyema.
Sekta ya afya nchini Zimbabwe imedorora na wahudumu wa afya hulalamika kwamba huwa hawalipwi vyema.
0 maoni :
Chapisha Maoni