Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MVUA DAR ZAFANYA MAAJABU, BWAWA LA MIAKA MINGI LAPATA UPENYO NA KUTENGENEZA MTO KUELEKEA BAHARI YA HINDI, LALETA MADHARA ZAIDI YA NYUMBA ZAIDI YA 50

Picha 10: Maajabu ya 'Beach Maiti' Bwawa kubwa lililohama usiku wa manane kutokana na mafuriko. Pata picha na video ya muonekano mpya wa eneo la 'Bwawa' hili na sasa ni Crater kuubwa ya kutalii

 

  
MPENDWA MSOMAJI: Matukio Blog ni mkaazi eneo la Kata ya Chamazi Mbagala linakopatikana bwawa maarufu la ‘kwa Mzala’.. bwawa maarufu kwa shuguli za Uvuvi wa Samaki aina ya Kambale, Perege, Mkunga, na aina nyenginezo nyingi na vijana wengi humiminika eneo hili kwa ajili ya kujipatia kipato kutokana na uvuvi na uuzaji wa Samaki. Pia Bwawa hili nimehusishwa na mambo ya kiimani kidogo, na wenyeji wa huku wamelibatiza bwawa hili na sasa linajulikana sana kama ‘Beach Maiti’ kutokana na kuwa hatarishi kwa maisha ya watu.. na imani inalihusisha bwawa hili na kiumbe aitwae Chunusi ambae ambae husemekana na kuondoka na roho ya mtu mmoja kila mwaka. Ndugu msomaji wa mkasa huu vuta hisia,.. bwawa hili ni kubwa sana na lenye kina kikubwa cha maji. Bwawa hili lina urefu usiopongua mita 300 na upana usiopongua mita 200, na sasa imebaki simulizi tuu.. Bwawa halipo tena eneo husika. Mkasa mzima umetokea juzi alfajiri ya kuamkia Alhamis tarehe 12/05/2017 wakati mvua zikiendelea bwawa likatafuta njia kwa kuvunja kingo zake na kutoweka ‘mazima’!!

Nyumba zisizopungua 20 na miti mikubwa aina ya miembe na minazi nayo ikapata njia na kutoeka na sasa eneo hili limekuwa sehemu ya Crater kuubwa inayovutia watu kwa mamia wanaofika kujionea kilichotokea na mandhari hii mpya.. Kwa picha zaidi na video tuwasiliane kwa namba: 0715722673 na 0786722673 Endelea kufuatilia blog yako yako ya Matukio na kuiunga mkono kwa kugonga ‘like’ halafu ‘share’ blessnewstz.blogspot.com

Nyumba hii ilibaki nusu mmiliki asijue la kufanya
Nimekuekea Video ya eneo husika, vuta picha hili eneo lilijulikana kwa jina la utani la 'Beach Maiti' kutokana na kuwa maji mengi msimu wote na kuwa hatarishi kwa maisha ya watoto wanaoshinda humo wakivua samaki.. ni maajabu hili bwawa limehama bila kubakia hata tone la maji.. ikikupendeza pata mda utembelee mahala hapa si mkasa wa kusimuliwa:



Sasa imekuwa Crater baada badala ya bwawa maarufu la kwa 'Mzala'

Baadhi ya majumba yaliyosalia baada nyumba nyengine nyingi kusombwa na maji

Maskini.. Watumiaji wa njia hii wakishangaa kukuta njia yao waliyoizoea haipo tena

Kabla tukio eneo lote hili lilikuwa katika usawa mmoja !

Wananchi wa kwa Mzala na wa maeneo mbali mbali walimiminika kwa wingi kushuhudia yaliyojiri

Njia ya maji ya sasa baada ya bwawa kuvunja kingo na maji yote kuvuja

Eneo hili zamani lilikuwa bwawa kubwa la uvuvi wa samaki aina mbali mbali

Eneo lililosombwa na maji ambalo awali yalikuwa makazi ya watu
CHANZO: tanzaniampya

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni