Haya kiduku kafanya mambo yake,
Watu wanaangalia habari za Korea Kaskazini kurusha silaha ya balistika wakiwa katika kituo cha treni Korea Kusini.
Korea Kaskazini imerusha kombora Jumapili katika anga za juu zaidi zisizo za kawaida katika njia inayopita silaha za balistika.
Hiyo ni dalili kuwa kunauwezekano kwamba Korea Kaskazini tayari iko
katika uwezo mpya wa teknolojia ya balistika inayoendeshwa na nguvu ya
nishati na mafuta yenye uwezo wa kupaisha kombora hilo mpaka kilometa
4,500.
Jaribio hilo kwa mujibu wa tamko la ikulu ya White House, “inalazimu kuwa ni ilani kwa mataifa yote kutekeleza vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.”
Mapema, Japan na Korea Kusini mara moja zililaani kitendo cha Korea Kaskazini na kusema kuwa ni tishio kubwa kwa eneo hilo na ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusiana programu ya silaha ya Korea Kaskazini..
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, aliagiza serikali yake “kuandaa hali zote za tahadhari,” kwa mujibu wa taarifa ya ofisi yake.
“Urushaji wa kombora hili la ballistika ni tishio kubwa kwa nchi zetu. Wizara ya Ulinzi na majeshi yetu ya ulinzi
yanaendelea kufanya kazi kwa karibu na Marekani na Korea Kusini katika
kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali,” Waziri wa Ulinzi wa Japan
Tomomi Inada amewaambia waandishi mjini Tokyo.
“Tutafanya juhudi zote tunazoweza kuhakikisha kuwa amani na usalama unakuwepo nchini kwetu.”
Waziri huyo amesema inawezekana kuwa aina mpya ya silaha ya balistika
ambayo imerushwa katika pembe ya sayari ya juu kabisa, ambayo imekwenda
umbali wa kilometa 2,000 na kuruka kwa dakika 30, kabla ya kurejea
katika pwani ya Japan baada ya safari yake ya kilometa 700.
Hata hivyo China imetaka pande zote kujizuilia ili kuepusha hatari inayoongezeka katika eneo hilo wakati Wizara ya Mambo ya nje ikitoa kauli ya kupinga kitendo cha Pyongyang kukaidi azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Beijing ni mshirika mkuu pekee wa Korea Kaskazini na ni nchi kuu inayofanya biashara na Pyongyang.
Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye hivi sasa yuko Beijing kwa ajili
ya mkutano wa kimataifa, ameeleza wasiwasi wake kuhusu jaribio la
kombora na kuongezeka kwa hatari, kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya
Kremlin.
Mahali lilipoangukiwa kombora hilo ni kilometa 400 kutoka pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini kwa mujibu wa serikali ya Japan.
CHANZO NI VOICE OF AMERICA . VOA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni