Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MSIKILIZE MAKONDA RC DAR ON LIVE STAR TV AKIJIBU MASWALI YANAYOHUSU TUHUMA MBALIMBALI



Watangazaji ni Leonard Mapuri na Aloyce Nyanda walioko Dar es Salaam na Samandu Hassan akiwa Studio za Mwanza.
Jina la Albert Bashite kwa kifupi alipoanza madawa ya kulevya ndio amaeanza kusikia majina mengi na kashfa za kifamilia na mali.

Ameulizwa Jina la Bashite amelianza kusikia kabla au baada ya vita ya madawa?
Makonda amesema swali hilo haliwezi kumsaidia yeye katika utendaji wake wala wananchi anaowaongoza.

Pia yeye na mkewe wameandika changamoto zilizojitokeza baada ya kuanza mapambano na watatoa kitabu kuhusu hilo.

Swali lingine ni liposali makanisa mawili hadi kulia alitikiswa na skendo za Bashite?
Makonda amesema kusali kwake na imani yake haiathiriwi na watu na alienda kwa sababu alikuwa akitimiza mwaka mmoja kama mkuu wa mkoa na aliona aanze na Mungu

Mwandishi anamuuliza lakini ni kwa nini alilia? Makonda anasema ukiwa unajadili kitu lazima uwe ndani ya kitu chake na mtu anayeamini anaposali anajua hisia anazopata mtu anapokuwa anasali.

Swali lingine: Na kuna watu walikuwa wanatuma mapepo kwake yakamgomea
Alitaja majina ya watuhumiwa wa madawa kwa kisasi na kuna watu wake wa karibu wanauza hakuwataja?

Makonda anasema cha kwanza ni kuelezeakwa nini aliingia kwenye vita ya madawa ndio alitakiwa aulizwe kwanza anasema alijifunza kwa miezi sita kuhusu biashara hiyo na kugundua kuna biashara za madawa yenye viwango vya juu na madawa yenye viwango vya chini.

Biashara hii inatesa familia nyingi na kufuta ndoto za vijana na yeye Mungu amampa nguvu za kupambana na wanaoua ndoto za vijana, pia ilani ya CCM inapinga matumizi ya madawa na pia sheria zilizotungwa na bunge zinapinga vikali matumiziya madawa

Anasema njia za kutaja majina ni kuwa alikuja nalo kwa kuwa lengo lake ni kupunguza madawa ya kulevya na sio kukakamata watu, ukitaka kukamata watu ndio utafanya kimyakimya.

Alipewa taarifa kutoka kwa wananchina vyombo vya serikali kuhusu wanaofanya biashara hiyo
Na walioitwa polisi ilikuwa ni priveledge kwao kwa kuwa iliwapa nafasi ya kujieleza na kujisafisha
Wapowatu waliojieleza na kukutwa na matatizo na wapo waliokiri wenyewe na kusaidiwa, wengine walikuwa hawajui maeneo yao yalikuwa yakifanyiwa biashara hiyo na wakaonyesha ushirikiano pia wapo wengi waliokamatwa bila kuitwa.

Yoyote yule nayesema aliitwa kwa kisasi ajiulize alikosana na Makonda wapi na Makonda ni taasisi sio mtu. Kwenye utumishi wa umma ana miaka 2 na miezi 4.

Swali lingine ni katika vita alinufaika yeye binafsi kwa kutumia matajiri na gari alizonazo ni moja ya mali alizojinufaisha nazo ana nyumba za kifahari Mwanza ana mali kiasi gani?

Makonda anajibu hizo n moja ya tuhuma alizopata ila alikua anaanza maisha kabla ya kuwa mtumishi wa umma ana maisha kabla ya ukuu wa wilaya na mkoa.

Na pia hilo sio kweli kuwa ana majumba na magari amewaalika waandishi wamtembelee nyumbani kwake na sio kila mali ataipata itakua ni ya kwake nyingine ni za umma

Kama kuna mtu wa madawa anakupa gari ili usimtaje halafu akupe gari wakati wanaohusika na kupambana ni serikali nzima na sio yeye atatokaje?

Na anaeleza kuwa kuna ushahidi kuwa njia aliyoitumia ya kutaja majina imepunguza madawa ya kulevya mtaani kuliko iliyokuwa ikitumika mwanzo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni