Hoteli yafungwa kwa madai ya kuuza nyama ya ng'ombe India
Mmiliki mmoja wa
hoteli katika jimbo la Rajasthan nchini India ameonyesha masikitiko yake
baada ya hoteli yake kufungwa kwa madai ya uwongo kwamba aliuza nyama
ya ng'ombe.
Maafisa wa Polisi siku ya Jumanne walisema kuwa vipimo
walivyochukua katika nyama iliopatikana katika hoteli hiyo ya Hayat
Rabbani mnamo mwezi Machi vilionyesha kwamba sio nyama ya ng'ombe, bali
kuku kulingana na gazeti la Hindustan Times.Ng'ombe ni wanyama watakatifu miongoni mwa jamii ya Hindu nchini India na kuna sheria kali dhidi ya uchinjaji na ulaji wa wanyama hao katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo ikiwemo Rajasthan.
''Kuanzia siku ya kwanza ,nimekuwa nikisema kuwa ni kuku lakini hakuna mtu mmoja aliyenisikiza'', alisema Naeem Rabbani.
''Ripoti hiyo pia ilithibitisha madai dhidi yetu ni ya uwongo''.
Hoteli hiyo ilifungwa baada ya kundi moja la kulinda ng'ombe kufanya maandamano mbele ya hoteli hiyo kwa saa kadhaa mnamo mwezi Machi, wakiimba nyimbo za kitaifa.
CHANZO: BBC SWAHILI
0 maoni :
Chapisha Maoni