ANGALIA VIDEO YA HALIMA BUNGENI ANASHANGAA WABUNGE WANAIPONGEZA SERIKALI
Mbunge wa Kawe Halima Mdee (CHADEMA) ni miongoni mwa Wabunge waliosimama leo Bungeni Dodoma na kutoa michango yao kuhusu Wizara ya Kilimo, mifugo na uvuvi.
Moja ya nukuu nilizozinasa kutoka kwake >>> ‘Nasikitika na ninawashauri tu Wabunge wapya na vijana, jukumu letu sisi ni kuisaidia Serikali na nchi… anasimama Mbunge anatoa pongezi kwa wizara ya kilimo kwa sababu ya hoja moja ya tozo‘
‘Jana Waziri katika hotuba yake anatumia robo tatu ya muda kusema tozo mbalimbali alizozikata badala ya kutuambia pamoja na hiyo tozo kukata, tuna mikakati gani mipana ya kusaidia asilimia 75 ya Watanzania?’
‘Hivi tungewekeza kwenye kilimo ipasavyo kama ambavyo mipango ya miaka mitanomitano kwa miaka zaidi ya 30 iliyopita, kama ambavyo ILANI ya CCM imekua ikisema kwa miaka zaidi ya 30 iliyopita….. ajenda isingekua tozo, tungeongeza kodi Serikali ingepata mapato sababu tuliwekeza vizuri’
‘Mimi natoka Jimbo la mjini, asilimia 85 mnatoka majimbo ya Vijijini…. mimi kwangu naathirika kwasababu tu ya mfumuko wa bei kwahiyo lazima nizungumze hapa sababu mwaka jana mfumuko wa bei ulikua 5.4 sasa hivi ni 6.4 kwa mujibu wa ripoti ya BOT iliyotoka juzi… sababu mahindi, sukari, mihogo imepanda bei‘
UNAWEZA KUMTAZAMA HALIMA MDEE KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
0 maoni :
Chapisha Maoni