Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MWONE RAIS MREFU KULIKO WOTE DUNIANI, KAGAME AKIONGOZA AFRIKA

[​IMG]
Kila siku watafiti wana habari mpya kuhusiana na maisha, tumeona tafiti nyingi zikifanywa zikiwemo za magari, majumba, watu maarufu.. Lakini sikuwahi kufikiri kwamba kuna siku nitakutana na utafiti unaozungumzia urefu wa Marais duniani.
Leo nakusogezea utafiti ambao ripoti yake ilitolewa January 4 2015 ambao unazungumzia marais 10 ambao ni warefu zaidi duniani:-



1. FILIP VUJANOVIC.
[​IMG]
Papa Benedict XVI akiwa na Rais wa Montenegro ambaye ndiye rais mrefu kuliko wote duniani, ana urefu wa futi 6.5.


2. NICOLAS MADURO
[​IMG]
Huyu ni Rais wa Venezuela, anashika nafasi ya pili kwa kuwa rais mrefu, ana urefu wa futi 6.3.


3. BASHAR AL- ASSAD
[​IMG]
Huyu ndiye Rais wa tatu kwa urefu duniani kutoka Syria, ana urefu wa futi 6.2



4. STEPHEN HARPER
[​IMG]
Huyu ni Waziri mkuu wa Canada, ana urefu wa futi 6.2


5. TOMAAS HENDRIK ILVES
[​IMG]
Huyu ni rais wa Estonia ambaye pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari, ana urefu wa futi 6.2


6. PAUL KAGAME
[​IMG]
Kwa Afrika huyu ndiye rais anayeongoza kwa urefu, lakini duniani anakamata nafasi ya sita kwa futi 6.2 huku binti yake akimzidi kwa kuwa na futi 6.6. Hapa Rais
Kagame alikuwa na Rais Obama na mkewe.


7. BARACK OBAMA
[​IMG]
Barack Obama ni Rais wa 44 ws Marekani, ana urefu wa futi 6.1 huku mke wake Michelle Obama akiwa na futi 5.11


8. DAVID CAMEROON
[​IMG]
Huyu alikuwa Waziri mkuu wa Uingereza, urefu wake haujatofautiana na wa Rais
Obama wa Marekani, wote wana futi 6.1


9. BLAISE COMPAORE
[​IMG]
Huyu alikuwa Rais wa Burkina Faso ambaye Oktoba mwaka 2014 aliamua kujiuzulu kutokana na machafuko nchini kwake, ana urefu wa futi 6. Hapa alikuwa na Rais Obama na wake zao.


10. RECEP TAYYIP ERDOGAN

Huyu ni rais wa Uturuki aliyekabidhiwa madaraka mwaka 2014, ana urefu wa futi 6


Chanzo : MillradAyo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni