TABOA YAKUBALIANA NA MAMLAKA NDANI YA SIKU 14
Wakati huohuo, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), leo imesema inayafanyia kazi madai
yaliyotolewa na Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (TABOA)
pamoja na Umoja wa Wasafirishaji wa Abiria jijini Dar es Salaam
(UWADAR). Hii ni siku moja baada ya vyama hivyo kutoa tamko la kutaka
kusitisha huduma ya usafirishaji kuanzia siku ya Jumanne.
Hata hivyo, SUMATRA kupitia Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa
Barabara, Johasen Kahatano imesema hakuna muswada wowote uliopelekwa
bungeni wala suala la kusomwa kwa mara ya mwisho kwa muswada wa sheria
inayotaka mmiliki wa gari kushitakiwa au kuhukumiwa kwa kosa alilofanya
dereva
“Hakuna kitu kama hicho, labda kama kuna kiongozi mwingine hapa katika mamlaka anayefahamu hilo, nitakupa namba ya simu ya Mkurugenzi Mkuu umuulize kama kuna jambo kama hilo,” alisema Kahatano.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe (katikati) akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea
kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na
mizigo nchini, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya
Mikoani (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed na kushoto ni Mwenyekiti wa
wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.
Vilevile alisema kuwa hajui wamiliki wa mabasi walikozipata taarifa za muswada huo na leo SUMATRA inaweza kuangalia nini cha kufanya kabla ya kuanza kwa mgomo wa mabasi hayo.
Wamiliki wa mabasi walitangaza kusitisha huduma za usafirishaji kuanzia
kesho jumanne ikiwa ni kwa lengo la kupinga sheria ya SUMATRA Sura ya
413 na ile ya Leseni za Usafirishaji Sura ya 317, inayotaka mmiliki wa
gari kushtakiwa au kuhukumiwa kwa kosa alilofanya dereva.
Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu akisoma mapendekezo yaliyotolewa kwenye
Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho alisema mgomo huo siyo wa mabasi
tu, unawahusu pia wasafirishaji wa malori pamoja na bajaji.
Hata hivyo wamiliki hao wa mabasi, leo walikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kuhusiana na namna ya kuyafanyia kazi madai yao.
Mkutano huo wa Waziri Mbarawa na TABOA umefikia makubaliano kuwa mgomo usitishwe na madai yao kushughulikiwa ndani ya siku 14.
0 maoni :
Chapisha Maoni