Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

JINA LA BASHITE LATUA RASMI KWA WAZIRI MKUU




Dodoma. Wabunge wa CCM wameitaka Serikali kutoa majibu sahihi bungeni kuhusu utambulisho wa mtu aitwaye Daudi Bashite.

Image result for kassim majaliwa images
WAZIRI MKUU  MHE KASSIM MAJALIWA
Sakata hilo liliibuka juzi katika kikao cha wabunge wa CCM kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini hapa.

Wabunge tofauti waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa, suala hilo lilihojiwa kwenye kikao hicho cha ndani ambacho hufanyika kabla ya mkutano wa Bunge kwa ajili ya kuwekana sawa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao walidai kuwa Serikali imeendesha na inaendelea kuhakiki vyeti vya elimu na baadhi ya watumishi wameshakumbwa na adhabu au kufukuzwa kazi kwa tatizo la vyeti feki.

Mpashaji mwingine aliiambia Mwananchi kuwa, Waziri Mkuu alijibu kuwa Serikali imepokea hoja hiyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Pamoja na kelele za watu tofauti kueleza uwezekano wa kughushi vyetu, si Baraza la Mitihani (Necta), Polisi wala Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliyojitokeza kuzungumzia suala hilo au kuchukua hatua.

Chanzo: Mwananchi

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni