Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
imeanza hatua za awali za uainishaji wa gharama,uandaaji wa mfumo
mbadala na upembuzi wa kina wa aina ya ubia ili kushirikiana na Sekta
binafsi katika utoaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa.
Hayo
yamesemwa leo bungeni na Naibu Waziri, Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Hamis Kigwangalla wakati akijibu hoja
mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Kufuatia
kukua kwa kasi kwa Sayansi na Teknolojia ya uchunguzi wa
magonjwa,Wizara inakubaliana na wazo hili juu ya kuangalia namna nzuri
ya kushirikiana na sekta binafsi katika utoaji wa huduma hizi,”Alisema
Mhe.Kigwangalla.
Amesema
kwa kuanzia sasa Wizara yake inafikiria kuanzisha ushirikiano kwa
kupitia ukodishaji wa vifaa ambapo Serikali itakodisha mashine hizo
ambazo zitakuwa za mbia na Serikali haitahusika na ununuzi,ufungaji na
matengenezo kinga ya mashine hizo.
Aidha
amebainisha kuwa katika mfumo huo,Wizara itakuwa na jukumu la kusimamia
utoaji wa huduma na itapata gawio lake kutokana na makusanyo yatokanayo
na uchangiaji wa huduma kulingana na mkataba.
“Ni
imani ya Wizara kuwa kutumia mfumo wa ubia na sekta binafsi(PPP) huduma
za uchunguzi wa magonjwa zitaimarika na kuipunguzia Serikali mzigo wa
gharama”,Aliongeza Mhe.Kigwangalla.
0 maoni :
Chapisha Maoni