Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

POLISI 8 WAHOFIWA KUUAWA NA MAJAMBAZI KIBITI


Image result for igp mangu images
INSPEKTA JENERALI WA POLISI TANZANIA ERNEST MANGU

Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi SABA wameuawa na majambazi huko Mkuranga, Mkoani Pwani.
Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.

Imeelezwa kwamba majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.

=====

UPDATES:

- Silaha zote (SMG) inadaiwa zimechukuliwa!

- Shambulizi limefanywa na mtu mmoja (jambazi/gaidi?)

=====

Came as a tip:
Jamani habari za usiku. Sisi huku BUNGU eneo la JARIBU mpakani tumepotelewa na askari saba(07) wa kikosi cha FFU.

Ilikuwa hivi:
Askari walikuwa wana-liviana ambapo section moja ilikuwa inatoka na nyingine inaingia. Sasa wakati hii inayotoka baada km 03, Jambazi/Gaidi lilikuwa limejificha porini karibu HIGHWAY baada ya gari kulikaribia jambazi/gaidi hili lilimshambulia dereva kwa mbele na gari kupoteza mwelekeo na kuanguka wakati huo jamba/gaidi liliendelea kushambulia.

Jambazi/gaidi alikuwa mmoja

=======

H. Crime Kibiti NR 62 MN 90 14/04/2017
Saa 02:30hrs kwa:
Upele Pwani (R) POL. Pwani (R) POL. Kibiti. Kbt/IR/337/2016.

Ilani ya kwanza

Kosa: mauaji (x)

Mnamo tarehe 13/04/2017 saa 18:15hrs huko Mkengeni kijiji cha Uchembe kata ya Mjawa tarafa na wilaya ya Kibiti (M) Pwani. Kundi la majambazi ambalo idadi yao bado haijafahamika wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la Polisi PT.3713 Toyota L/Cruiser na kuua askari nane ambao ni

1. A/INSP Peter Kigugu

2. F.3451 CPL Francis

3. F.6990 pc Haruna

4. G.3247 pc Jackson

5. H.1872 PC Zacharia

6. H.5503 PC Siwale

7. H.7629 PC Maswi

8. H.7680 PC ayoub.

Pia walimjeruhi askari no F. 6456 PC Fredrick kwa kumpiga risasi ya mkono wa kushoto na amepelekwa hospitali ya misheni Mchukwi kwa matibabu.

Baada ya majambazi hao kufanya mauaji kwa askari walifanikiwa kuchukua silaha tisa kati ya hizo SMG sita zikiwa na risasi 30 kila moja na long range tatu.

Awali gari ya polisi ilikuwa ikitokea Jaribu mpakani kwenye road block kuelekea Bungu, baada ya kubadilishana na shift nyingine ndipo walipofika maeneo ya Mkengeni sehemu yenye mteremko na majani marefu na kuanza kushambuliwa na najambazi kwa kupigwa risasi kioo cha mbele usawa wa dereva na kusababisha dereva kupoteza uelekeo na gari kuingia kwenye mtalo wa barabara na ndipo majambazi hao kufanya mauaji kwa askari.

Baada ya tukio hilo mahojiano yalifanyika na watuhumiwa waliokuwa wakishikiliwa na polisi ambao majira ya 02:15 hrs walienda kuonyesha eneo la msitu wa Kilima cha Mianzini barabara ya Nyamisati ambalo wahalifu hao hujificha.

Walipofika maeneo hayo walishambuliwa na majambazi hayo na kuwajeruhi wenzao waliokuwa mbele kwenda kuonyesha na baadaye walifariki dunia na ndipo majibizano ya risasi yakaendelea baina yao na polisi.

Katika majibizano ya risasi majambazi walifanikiwa kukimbia na kutelekeza silaha nne kati yao mbili za polisi aina ya polisi zenye no. Smg tzpl 10549 risasi 30, smg tzpl 26881630 risasi 30 na silaha mbili za majambazi smg moja na sar moja.

Eneo la tukio limekaguliwa na DCP Kashai, DCP Sabasi, SACP Mayala, ACP Ngoyayi, SSP Canute Msacky OCD - Kibiti na ASP Juma Kanena OC - CID Kibiti.

Miili ya marehemu imepelekwa hospitali ya taifa Muhimbili.

FCR/Maendeleo zinafuata.

Mwisho///////// toka: Crime (W) Kibiti

=======

IKULU, Rais Magufuli alaani mauaji ya Askari polisi 8 huko Kibiti mkoani Pwani. Ampa pole IGP na Askari wote kwa kuwapoteza wenzao.

Habari zaidi soma=>Rais Dkt. John Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa IGP na familia za Askari wote waliouawa


Bams said:
Tunaambiwa nchi ipo salama lakini ukweli ni kuwa hatupo salama kama tunavyoaminishwa. Akiliyangu inanituma kuwa huu siyo ujambazi. Jambazi alikuwa anatafuta nini kutoka kwa askari? Tumeambiwa silaha zote zimebebwa, zimepelekwa wapi? Matukio ya namna hii yanazidi kuongezeka. Kuna kitu kinaendelea nchini mwetu ambacho wengi hatujui lakini nina imani serikali inatambua.

Rais Magufuli, kwa namna yoyote, tafuta uwezekano wa wananchi kushikamana. Huwezi kumshinda adui ikiwa wananchi mmepasuka vipande vipande. Jitihada zifanyike ili wananchi wavipende vyombo vyao vya uĺinzi na usalama, na wavisaidie kupata taarifa zinazosaidia ulinzi wa Taifa na usalama wa askari na wananchi wote. Hatuwezi kumkabili adui ikiwa hatuna mshikamano.

Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipeleke nguvu zao zote kwenye usalama wa Taifa letu kuliko kwenye mambo madogo yasiyo na madhara makubwa kwa Taifa lakini yenye kupunguza mshikamano wetu.

Si jambo jema kupuuza maisha ya mtu hasa pale anapokuwa ameyatoa kwaajili ya maisha ya wengine. Taifa linahitaji askari na kila mtu anahitaji ulinzi wa askari. Wanapokuwepo askari waliopoteza maisha, tena wakiwa kazini, kazi ya kuhakikisha usalama wa nchi ni vema kutambua mchango wa binadamu wenzetu katika Taifa hata kama kuna mapungufu.


Source: Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni