Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MAUAJI YA ASKARI POLISI 8 SI LA KIGAIDI BALI UJAMBAZI " KAMISHNA NSATO MARIJANI"

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani ameongea na waandishi wa habari mchana huu na kutolea ufafanuzi tukio la mauaji ya Askari Polisi 8 lililotokea jana jioni huko Kibiti, Pwani.
Image result for kamishna nsato marijani images
KAMISHNA WA JESHI LA POLISI TANZANIA NSATO MARIJANI

CP Marijani ameeleza kuwa tukio hilo sio la kigaidi kama ambavyo imekuwa ikivumishwa, bali ni tukio la kawaida la ujambazi ambalo halililazimu Jeshi la Polisi kuunda Kanda Maalumu ya Kipolisi kwa Mkoa wa Pwani.
Aidha, amesisitiza kuwa, hilo ni tukio la kawaida na wala sio tukio la kutisha na kuzua hofu bali imetokea tu bahati mbaya mapolisi kuuawa na wao kama Jeshi Imara watazidisha mapambano na kudumisha ulinzi.

Mpaka sasa, wameshajibu mashambulizi yaliyowalaza chini majambazi 4 na idadi yao itaongeza kwa kuwa imeundwa operesheni maalumu ambayo haitokuwa na mzaha wala msamaha.

Msikilizeni zaidi kwenye video hiyo hapo chini.. 


Source: Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni