MUNGU MKUBWA, AJALI YA BOTI ZANZIBAR WAVUVI WOTE 53 WAMESALIMIKA
Wavuvi wengine kumi wameokolewa leo wakiwa hai na kufanya idadi ya wavuvi wote 53 kusalimika kifo baada ya boti yao ya uvuvi kupinduka ikiwa baharini.
Akitoa taarifa rasmi msemaji wa mamlaka ya usafiri baharini Zanzibar Bi.Shekha Ahmed Mohamed amesema baada ya zoezi la jana ambalo wavuvi 43 waliokolewa leo hii taasisi za uokozi zimefanikiwa kuwaokoa wavuvi nane waliokutwa ufukweni mwa kisiwa cha Tumbatu na watatu hali zao hazikuwa nzuri na wamefikishwa hopitali ya mkoa ya Kivunge.
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha mamlaka ya usafiri baharini Pandu Juma Pandu amesemea wao sio wanaotoa leseni za boti hizo na hivi sasa mchakato umeanza ili kuhakikisha leseni hizo zinatolewa kwa pamoja na idara ya uvuvi na mamlaka ili kunusuru ajali.
Hii ni mara ya kwanza kwa ajali kubwa ya baharini kwa idadi kubwa ya wananchi 53 wote kunusurika kifo ambapo baadhi yao wamekuwa waliogolewa baharini kwa masaa zaidi ya masaa 24, ingawa bado kilio kikubwa cha wananchi ni kuona serikali inaweka miundombinu imara ya haraka na ya uokozi.
Chanzo: ITV
0 maoni :
Chapisha Maoni