Watu 8 waliovalia ninja wamevamia mkutano wa chama cha CUF na kujeruhi baadhi ya waandishi wa habari na wafuasi wa chama hicho Mabibo Dar Es Salaam,
Wakuu kulikuwa na mkutano wa CUF ya upande wa Maalim Seif,ulipangwa kufanyika katika hotel ya Vina-Mabibo.
Ghafla wakavamia watu waliovaa mask usoni na kuanza kutembeza kichapo kwa waandishi wa habari na wanachama waliokuwepo eneo la tukio.
Wavamizi hao walikuwa na mapanga,marungu na mmoja akiwa na bastora.
Hali iliyosababisha mkutano kusambaratika na watu kukimbia hovyo,nina mtu katika eneo la tukio,ananipa habari kuwa kichapo kimetokea na baadhi ya watu kujeruhiwa.
Picha hii juu ni mmoja wa wavamizi,ambaye wakati anataka kutoroka,wananchi walimdhibiti na kumpa kichapo.
More News to come.....
0 maoni :
Chapisha Maoni