Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MALINZI AMFUKUZISHA KAZI MTANGAZAJI WA RADIO TIMES FM

Kuna taarifa inasema Mtangazaji nguli wa michezo hapa nchini na aliyepata kuwa msemaji wa Club ya Simba Clifford Mario Ndimbo amefukuzwa Radio Times Fm ambapo ndio alikuwa akiendesha kipindi chake cha michezo kiitwacho "Wizara ya Michezo"


Taarifa za ndani zinasema kuwa Mkurugenzi wa radio hiyo amefikia hatua hiyo kwa kile kinachosemekana kuwa ni kulinda maslahi ya viongozi wa michezo hasa mpira wa miguu waliokuwa wakianikwa hadharani "uozo" wao kupitia segment ya "Dokodoko" ambayo ilijikita katika kueleza ukweli wa masuala mbalimbali ya mpira wa Tanzania.

Wafuatiliaji wa kipindi cha Wizara ya michezo wanasema wana muda mrefu sana hawajasikia segment ya "Dokodoko" ambayo ndio iliibua skendo kubwa ya Rushwa TFF na mambo mengine, na kupelekea kesi kwenda mahakamani na TFF wakashinda.

Washabiki wa kipindi hicho wanasema kwa siku tatu sasa hawajamsikia Ndimbo hewani na kipindi kinaendeshwa na Mtangazaji mwingine huku kikiwa na sura tofauti na kupoteza mvuto.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Ndimbo aliandika "Dokodoko Next Destination loading......" akiwa na maana kipindi chake sasa kinahama na kwenda radio nyingine, hili linathibitisha uvumi huu ulioanza kusambaa tangu wiki iliyopita.

Watu wanaamini mkurugenzi wa Times Fm ametumiwa na baadhi ya viongozi wa mpira ili alinde maslahi yao bila kujua anaharibu Radio yake mwenyewe na kuvunja heshima iliyojijengea.

Safari ya mpira wadau ni ndefu sana sitashangaa nikisikia vipindi vya michezo vinatangaza matokeo tu, maana mpaka wakurugenzi sasa wanatumika kwa njama za hawa majamaa... Hiyo Times radio mimi ndio sisikilizi tena maana boss mwenyewe hajielewi, badala ashangilie na kuwapa sapoti watu wake, yeye ndio anawafukuza.

Hili suala kama Malinzi kaweka mkono wake itafahamika tu, lakini lazima ajue watu wa mpira tumemchoka, aondoke zake na rushwa zake !! Alitumia media wakati anaingia, naona sasa tena kamuweka Kwapani Mkurugenzi wa Times Fm ili atumie Radio yake kuingia kwa kudhoofisha makali ya kipindi cha michezo.

Wanamichezo na wapenda mabadikiko bado tutamkumbuka mzee wa "Dokodoko" Clifford Mario Ndimbo na team yake, na popote mnapokwenda ninaamini mtaendelea kusimamia haki na kusaidia kuokoa michezo nchini. Tanzania nzima inajua kazi yenu, watanzania wanajua bila nyinyi ile skendo ya upangaji matokeo ingekuwa ni siri, mmeonesha mwanga kwa watangazaji wengine wa vipindi vya michezo na watajifunza kupitia nyinyi.

Watu wa mpira sasa tuna haja gani ya kusikiliza michezo ya radio kama Times? Michezo itakayokuwa inachujwa ili kumfurahisha Malinzi na watu wake.. Yaani baada ya kushinda kesi tu ndio yanatokea haya ?? Dokodoko haipo tena, na Ndimbo hayupo tena !! Mwisho wenu unakaribia.


Source : Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni