THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
SHAURI LA MADAI YA WIZI WA FEDHA ZA RUZUKU YA CUF KATI YA THE REGISTERED
TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) DHIDI YA
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI (JAJI FRANCIS MUTUNGI) NA MWANASHERIA
MKUU WA SERIKALI:-
LEO Tarehe 20/4/2017 mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera
kulikuwa na mashauri matatu yaliyoletwa pamoja yanayohusiana na maudhui
tajwa hapo juu.
Miscellaneous Civil Application (Maombi madogo Shauri namba 28/2017) –
linahusiana na Amri ya Mahakama kuzuia Lipumba na kundi lake wasipewe
fedha za Ruzuku ya CUF.
Civil Application (Maombi Shauri la msingi namba 21/2017) – Linahusiana na CUF kupinga na kuhoji uhalali wa Msajili kutoa
kiasi cha fedha za Ruzuku shilingi Milioni 369 kwa Lipumba na kundi lake
kinyume na taratibu za fedha na mamlaka halali ya uongozi wa CUF Taifa.
Miscellaneous Civil Application (Maombi madogo shauri namba 34/2017- inahusiana na Profesa Lipumba na Thomas Malima kuomba kuingizwa katika kesi hiyo kwa madai kuwa wana maslahi mapana na shauri hilo.
Maamuzi;
• Mahakama imekubali ombi la Mawakili wasomi Juma Nassor na Hashim
Mziray la kuitaka Mahakama Kuu kuongeza muda wa zuio lililotolewa hapo
awali (To extend time of Interim Order) la kuzuia fedha za Ruzuku ya CUF
kutotolewa kwa Lipumba na wenzake mpaka hapo mashauri hayo
yatakapomalizika. Aidha, upande wa Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameweka pingamizi la kuendelea na shauri hili kwa madai kuwa Bodi ya Wadhamini ya CUF iliyofungua shauri hilo siyo halali (invalid Board)
• Kuhusu Ombi la Lipumba na Thomas kuingia katika Shauri hilo Mahakama imepokea maombi hayo na kwa kuwa
hawajawasilisha nyaraka hizo kwa CUF na walalamikiwa wengine, Mahakama
imeagiza nyaraka hizo ziwafikie wahusika (To be Saved) kabla ya Tarehe
6/6/2017 ili zijibiwe. Hata hivyo, yameonekana makosa ya uandaaji wa
Nyaraka hizo zilizoandaliwa na Lipumba na Thomas kwamba wao ni waombaji
(Applicants) lakini wamejiorodhesha katika sehemu ya walalamikiwa (Respondents) ambayo ni makosa kisheria.
• Shauri la Msingi namba 21/2017 lililopangwa kusikilizwa Tarehe 24/4/2017 sasa limepangwa kusikilizwa pamoja Tarehe 6/6/2017
• Kutokana na Mashauri yote haya kuwa na muelekeo unaofanana (Similar but not the same cause) Mheshimiwa Jaji Dyansobera ameshauri yakusanywe pamoja (Joint Trial Consolidation) ili yaende sambamba katika kusikilizwa na kutolewa maamuzi yake. Ombi/ushauri ambao utafanyiwa kazi kisheria na Mawakili wetu kuona namna ya kuyaendea masuala hayo baada ya kupokea Nyaraka toka kwa wahusika. Ni kwa msingi huo Mashauri yote yamepangwa kutajwa na au kusilikizwa Tarehe 6 June, 2017 baada ya pande husika kupokea nyaraka husika (Necessary Documents) na kuzijibu ndani ya muda huo.
• Kwa Upande wa Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliwakilishwa na Mawakili wasomi Mhe. Hachi Chang’a na Mhe. Paulina Bendeni na Upande wa waleta maombi mapya (Lipumba) waliwakilishwa na Thomas Malima (Bila Wakili yeyote), ambapo tofauti na wakati mwingine leo kulikuwa na utulivu na kuzingatia Nidhamu ya Mahakama.
Nichukue fursa hii kuwajulisha Wana-CUF na Wapenda mabadiliko wote nchini kuwa Mawakili wetu wanatuwakilisha vyema na masuala yote yako sawasawa na kwamba upangwaji wa Tarehe za Shauri hilo umezingatia taratibu zote za kisheria na majukumu mengine ya Jaji/Mahakama.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
MAHARAGANDE
NMHUMU
maharagande@gmail.com
0715062577/0784001408
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni