Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

GAZETI LA UHURU LAFICHUA SAKATA LA MCHANGA


Katika mambo yanayotugharimu watanzania ni msemo wa "yaliyopita si ndwele tugange yajao"
Kumekuwa na makosa mengi ya kuligharimu taifa yakifanywa na viongozi ambao tumekuwa tukiwapa dhamana ya kuongoza nchi yetu, lakini sijawahi kuona wakiwajibishwa.

Wanaingia, wanatawala wanaharibu wanaondoka anayekuja vilevile. Katika mambo ambayo nilimtegemea sana JPM katika ukweli wake ni kuwa mkweli kama ambavyo amejinadi toka wakati wa kampeni kuhusu kiini cha tatizo kuwa ni mikataba mibovu watangulizi wake kwa yote waliyoingia. Badala yake na yeye analalamika tu, fikiria kama ingekuwa wapinzani ndio walitawala miaka mitano ilopita, kama namuona Rais wangu ambavyo angewafanya.

Suala la mchanga wa dhahabu kwa mfano, hivi Rais wa awamu ya nne na tano wanachomokaje hapa? Gazeti la uhuru la leo limesema ukweli kama linavyojinadi "ukweli daima", kwamba makontena ya mchanga yameshauzwa nje kuanzia 2001 hadi 2016. Hii inamaana wakati wa utawala wa Rais Mkapa na Kikwete, maana yake kwa kipindi chote hiki tumeongozwa na ama na watu kwa maslahi yao binafsi au kwa kiburi cha "Tutawala milele" hivyo tuijitajirishe tu. Kama hadi kufikia gazeti la uhuru kuandika haya mangapi yanayopigiwa kelele za ukweli mfano escrow hayaandikwi?

Watanzania tunasubiri nini? Tubadilishe watu wa kutuongoza na kusimamia kodi zetu.
Nilikuwa na imani na JPM lakini simwelewi kabisa, analalamika kuhusu mchanga kwanini asiseme kweli kama lilivyoandika uhuru kwamba serikali za chama chake ndizo zilizotufikisha hapa yeye akiwa waziri? Cha ajabu hata alikuwa haoni wakti huo angetusaidia kutoa hoja binafsi labda.

Kama nguvu nyingi inatumika kuwashughulikia akina Mbowe anayedaiwa kutolipa kodi, Manji anayedaiwa kuajiri wageni bila vibali, wanaokosoa serikali na kuhoji mambo mbalimbali ya viongozi, wanaokwenda tofauti na chama tawala kwa nini tusitumie nguvu hiyo pia kuwawajibisha viongozi wetu hawa waliotutia hasara kwa miaka karibia 17 sasa ili hata yeye na wajao wajue wakiharibu watawajibishwa?

Jamani, tusiogope kubadilisha serikali na kuwapa wapinzani nchi tuwe kama Ghana, Zambia etc, sioni tofauti ya uwezo wa wanaotwala sasa na wapinzani, naweza sema wako watu makini zaidi upande wa upinzani, mfano Zitto, Tundu Lissu just to mention few. Kufanya hivi kutaleta discipline kwa kila tunaowapa dhamana, wataongoza kwa matakwa ya tuliowachagua wakijua hawana uhakika wa kutawala tena na pengine kushtakiwa kama wakiharibu na sio kwa fikra zao kama ilivyo sasa.

Wapenzi wa vyama msichafue hali ya hewa please.
uhuru-Leo-03-04-2017.jpg
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni