Daktari wa maradhi ya moyo Mtanzania atambuliwa Marekani,
Daktari mshauri mwandamizi wa
magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro, nchini
Tanzania amepewa tuzo na Chuo Kikuu cha Magonjwa ya Moyo Marekani
(American college of Cardiology).
Dkt Harun Emalda Nyagori ambaye
pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis, amepewa tuzo ya
kutambuliwa kwa utafiti na uzoefu wake katika ushauri kuhusu magonjwa ya
moyo barani Afrika.Baadhi ya utafiti uliofanywa na Dkt Nyagori ni pamoja na kushindwa kufanya kazi kwa dawa za maradhi ya moyo nchini Tanzania na changamoto za magonjwa ya moyo nchini humo.
Tuzo nyingine alizopata ni kutoka kwa Jumuiya ya madaktari bingwa wa maradhi ya moyo barani Ulaya na Jumuiya ya Umoja wa Madaktari bingwa wa maradhi ta moyo nchini Mexico.
Dkt Nyagori ni kati ya madaktari bingwa wachache nchini Tanzania wanaoshauri na kutibu maradhi ya moyo yasiyohusiana na upasuaji.
Dkt. Nyagori pia aliwahi kupokea tuzo nyingine. Septemba 2015 alipokea tuzo kutoka Jumuiya ya Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo Barani Ulaya, London.
Tuzo nyingine ni kutoka Jumuiya ya Umoja wa madaktari bingwa wa maradhi ya Moyo nchini Mexico mwaka 2016.
Kwa kushirikiana na madaktari wengine, Dkt Nyagori amekuwa akiwatibu kwa wastani wagonjwa 40 hadi 60 kwa siku.
Idadi inayofikia wastani wa wagonjwa 160 - 200 kwa wiki.
Source: Jamii Forum
0 maoni :
Chapisha Maoni