Marekani yakatiza ufadhili kwa UNFPA linalohusika na mpango wa uzazi
Marekani imesitisha ufadhili kwa
mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu, UNFPA unaotoa msaada kwa
ajili ya mpango wa uzazi kote duniani.
Hatua hiyo italifanya
shirika hilo la Umoja wa Mataifa kupoteza takriban dola milioni
thelathini za ufadhili kwa mwaka huu pekee. UNFPA limepinga madai kuwa linafadhilili shughuli za uaviaji mimba.
- Trump kuteua jaji anayepinga uavyaji mimba
- Uavyaji mimba: Wachangisha fedha kupinga sheria ya Trump
- Trump hayuko juu ya sheria, jaji asema
BALOZI WA MAREKANI NIKKI HALEY MSIMAMIZI WA USITISHAJI UFADHILI |
Hii ina maana kuwa UNFPA litapoteza ufadhili wa siku zijazo zikiwemo dola milioni 32.5 zilizokuwa zimepangwa kutumiwa mwaka huu.
Wizara ya mambo ya nje Marekani inasema kuwa uamuzi huo ulizingatia shughuli za UNFPA za mpango wake wa uzazi na serikali ya Uchina, ambazo inasema ulisaidia kuavya mimba na kufunga uzazi kwa lzima.
Badala yake ufadhili huo utaelekezwa katika mipango mingine ya uzazi katika nchi zinazoendelea.Shirika hilo hatahivyo limesema kuwa madai hayo ''si sahihi'', na kwamba kazi zake zote zimekuwa ni za kuboresha haki za kibinfasi na wanandoa kuchukua maamuzi yao bila ubaguzi.
Source: Swahili BBC UNFPA
0 maoni :
Chapisha Maoni