Bei ya mafuta yaongezeka Tanzania,
Mamlaka ya Udhibiti
wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta ya
petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoaanza kutumika kuanzia leo.
Akitangaza
bei hizo leo Meneja wa Mawasiliano wa Ewura nchini Tanzania , Titus
Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka kwa Sh 3 na itauzwa
kwa Sh 2057 kutoka 2060, dizeli imepanda kwa Sh 12, kutoka Sh 1913 hadi
1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka 1952."Mabadiliko haya bei yametokana na bei za mafuta katika soko la dunia kubadilika sanjari na mfumuko wa bei na gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita,"amesema Kaguo.
Source : Swahili BBC London
0 maoni :
Chapisha Maoni