Sarafu ya dhahabu ya $4m yaibiwa Ujerumani,
Sarafu kubwa iliyotengenezwa kwa dhahabu, ambayo ina picha ya Malkia Elizabeth wa Uingereza, ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya $4m (£3.2m), imeibiwa kutoka kwenye makumbusho Ujerumani.
Sarafu hiyo kutoka Canada imeandikwa kuwa ya thamani ya $1m, lakini kwa sababu imetengenezwa kwa kilo 100 za dhahabu, thamani yake ni ya juu sana kwa kutumia bei ya sasa ya dhahabu.Iliibiwa usiku kutoka makavazi ya Bode mjini Berlin.
Haijabainika ni vipi wezi walifanikiwa kuingia bila kugunduliwa na mtambo wa kuzuia wezi, na kisha wakafanikiwa kutoroka na sarafu hiyo ambayo nusu kipenyo chake ni cha nusu mita.
- Mhubiri apata almasi ya mamilioni ya dola Sierra Leone
- Mke wa Mugabe aamrishwa kurudisha nyumba tatu
Sarafu hiyo inadaiwa kuwa nzito sana kiasi kwamba mtu mmoja hawezi kuibeba.
Polisi wa eneo hilo wanasema huenda polisi waliingia kupitia dirisha.
Ngazi ilipatikana imetupwa kwenye reli iliyo karibu, msemaji wa polisi Winfrid Wenzel aliambia Reuters.
"Sarafu hiyo ilikuwa imehifadhiwa ndani ya sehemu isiyoweza kupenya risasi ndani ya makumbusho," alisema.
Sarafu hiyo ilifuliwa mwaka 2007 na Royal Canadian Mint.
0 maoni :
Chapisha Maoni