Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

UWANJA WA NDEGE WAITWA CRISTIANO RONALDO AIRPORT


Ureno: Cristiano Ronaldo kupata uwanja wa ndege

Ronaldo
Ronaldo alifunga bao lake la 71 kimataifa na kumfikia Mjerumani Miroslav Klose

 

Cristiano Ronaldo alifunga bao kwenye mechi iliyochezewa katika kisiwa alikozaliwa cha Madeira, siku moja kabla ya uwanja wa ndege katika eneo hilo kupewa jina lake.
Ureno hata hivyo, walitupa uongozi wa mabao mawili na mwishowe wakalazwa 3-2 na Sweden.
Urengo walikuwa wanaongoza kupitia bao la 71 la Ronaldo katika michuano ya kimataifa, pamoja na bao la kujifunga na Andreas Granqvist.
Lakini Viktor Claesson alifunga mawili naye Cavaco Cancelo kajifunga dakika za mwisho mwisho na kuwapa Sweden ushindi.
Ronaldo anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya kuupa uwanja huo jina lake Jumatano.






Madeira
Picha ya Ronaldo ilitungikwa katika uwanja wa ndege wa Madeira wiki hii

 

Ronaldo, 32, anayechezea Real Madrid, aliongoza taifa lake kushindwa ubingwa wa Ulaya mwaka jana.
Alizaliwa katika mji mkuu wa Madeira, Funchal na baadaye akachezea Sporting Lisbon na Manchester United.
Baadhi ya wanasiasa wa eneo hilo wamepinga uamuzi wa kubadilisha jina la uwanja wa ndege wa Madeira kuwa Uwanja wa Ndege wa Cristiano Ronaldo.
"Wakati mwingine, shukrani za taifa huwa hazidumu sana, lakini Madeira haitasahau," Miguel Albuquerque, rais wa serikali ya Madeira alitangaza, hatua ya kubadilisha jina la uwanja huo ilipotangazwa.

 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni