Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

JE, KAFUMU NA MUHONGO HILI SWALA LA MCHANGA MNALIFAHAMU?


MHONGO NA KAFUMU......
Mnaifahamu hii....??

Geologist Abdul ambaye kafanya kazi Migodi ya ACACIA, Bulyanhulu, North Mara ambaye kwa sasa yuko Afrika ya Kusini kama mtaalamu wa makampuni ya huko aliulizwa maswali kuhusu ukweli wa hii sakata la mchanga unaosafirishwa nje ya nchi.Aliandika yafuatayo:

Mawe yanapotoka kwenye shimo yanapelekwa processing plant. Yanapondwa pondwa (crushing and milling).

Baada ya hapo kwa Geita, yanafanyiwa gravity concentration (sawa na kuchekechwa, mazito yanakaa chini, mepesi yanakaa juu). Gravity concentration inafanywa kama dhahabu ni free gold (yaani grain size yake ni kubwa). Kama ni fine gold (yaani dhahabu ina grain size ndogo sana) basi inachanganywa na cyanide baadae wanafanya carbon-in-leach (kuyeyusha hiyo dhahabu halafu inavutwa na carbon maana carbon ina attract dhahabu vizuri tu). Baadae wanachukua hizo carbon zilizojaa dhahabu, wanazichoma kutoa dhahabu na kutengeneza gold bars
Ninavyojua kwa Buzwagi na Bulya, 70% ya dhahabu inakuwa recovered sawa na hiyo process ya geita. Kwa hiyo 70% ya dhahabu ya Buzwagi na Bulya wanapata dhahabu pure 97% gold hapo hapo site
30% ndio issue sasa. Maana imechanganyikana na copper na silver. Kwa hiyo wanachofanya wanafanya floatation ili concentrate gold, copper na silver.
Migodi ya Geita na North Mara, dhahabu inasafishwa palepale. Yaani wanachimba, inapelekwa processing pale pale mgodini hadi wanapata gold bars (dhahabu pure to almost 98%).

Migodi ya Buzwagi na Bulya, mawe yake ni tofauti kidogo na yale ya Geita na North Mara. Maana yana dhahabu, copper na silver
Kwa hiyo Bulya wanachimba takriban tani milioni moja kwa mwaka. Wakifanya hiyo floatation wanaiconcentrate hadi inabaki tani elfu ishirini na tano tu. Punguzo la zaidi ya 40 (1mil divide by 25000).

Kwa Buzwagi, wanachimba tani milioni nne kwa mwaka, wakifanya hiyo floatation), wanabaki na tani elfu ishiri na tano pia. Punguzo la zaidi ya 200.

Sasa hizo tani elfu hamsini ndizo zinazosafirishwa kwenda nje kwa mwaka (tani elfu ishirini na tano za Bulya na similar amount kutoka Buzwagi)
In summary katika mapato yote ya Bulya na Buzwagi, mapato asilimia 70 yanapatikana hapo hapo site bila kupeleka kwa smelters wa nje ya nchi. Na mapato yao asilimia 30 ndio yanatokana na hiyo michanga (concentrate) inayosafirishwa nje. Kati hiyo 30%, asilimia 25 ni mapato kutoka gold na asilimia tano ni copper na silver.

Kusema Bulya na Buzwagi wanasafirisha tani milioni moja ya concentrate nje ya nchi sio sahihi.
Na kabla ya kusafirisha nje, TMAA (Tanzania Minerals Audit Agency), MEM (Ministry of Minerals and Energy), pamoja na TRA wanahakiki kuwa kilichoripotiwa ndio kinachosafirishwa, wanaweka na mihuri yao. On top of that, kuna samples zinachukuliwa kila layer (kuna layers kadhaa kwenye contena) zinapelekwa laboratory kuhakiki. Zinapelekwa laboratory tatu na results kutumwa kwa kampuni, TMAA, MEM na TRA. Wakisharidhika wote, ndio royalty inalipwa na mzigo kusafirishwa
Gold sales zao ni asilimia 95 zinatokana na gold, asilimia tano ni copper na silver. Kati ya hizo 95%, asilimia 70 ya gold sales inasafishwa onsite na asilimia 25 ya gold ndio inasafirishwa nje kwa smelters pamoja na hiyo asilimia tano nyingine ambayo ni copper na silver
Smelters wa hiyo michanga wapo Germany, China na Japan.

Tukisema Tanzania tujenge smelting plant hapo, ili hiyo asilimia 30 ya mapato ya Bulya na Buzwagi yasafishwe hapo hapo Bongo, lazima tuwe na uwezo wa kushindana na wachina, wajapani na wajerumani. Maana kutegemea mzigo wa Buzwagi na Bulya hautatosha kuendesha hiyo smelting plant. Buzwagi wamebakiza miezi 12 tu kumaliza hiyo michanga inayosafirishwa, meaning itabakia Bulya tu ndio itakayokuwa inatoa hiyo michanga....tani elfu 25 kwa mwaka.
Ndio maana nasema mkuu sijui kama anapewa ushauri mzuri, au watu wanaogopa kumshauri
Hivyo lazima tuwe na uwezo kwa ku compete ili tupate michanga kutoka nje. Sijui tuta compete vipi wakati umeme wetu ni ghali kuliko umeme wa china na Germany. Vile vile smelters wanapewa masharti kuwa lazima utoe 97% pure gold au copper. Ikishuka hapo unapigwa penalty.


Source: Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni