Kupunguza kiwango cha chumvi huzuia mtu kwenda chooni usiku
Watu ambao huamka usiku kwa minajili
ya kuenda chooni, wanahitaji kupunguza kiwango cha chumvi katika
chakula chao, kwa mujibu wa madaktari nchini Japan.
Tatizo hilo
linalofahamika kama nocturia, ambapo mara nyingi huwaathiri watu walio
na zaidi ya miaka 60, husababisho matatizo ya kupata usingizi na
linaweza kuathiri maisha ya mtu.Uchunguzi huo uliofanyiwa zaidi ya watu 300 wa kujitolea, uligundua kuwa kupunguza kiwango cha chumvi kwenye chakula, humwezesha mtu kupunguza safari za kuenda haja ndogo.
Watafiti kutoka chuo cha Nagasaki , waliwasilisha matokeo yao kwenye warsha moja ya sayansi mjini London.
Walichunguza wagonjwa waliokuwa wakitumia kiwango kikubwa cha chumvi pamoja na matatizo ya kulala kwa miezi mitatu baada ya kuwapa ushauri wa kupunguza kiwangi hicho kwenyeychakula chao.
Safari za kuenda chooni zilipungua kwa zaidi ya mara mbili kila siku hadi safari moja.
Hiyo pia ilishuhudiwa mchana na maisha ya watu hao pia yakaimarika.
Hitaji la kuamka usiku kwa haja ndogo huwaathiri zaidi ya nusu ya wanaume na wanawake walio na zaidi ya miaka 50.
Hali hiyo ni kawaida kwa watu wazee ambao wengi wao huamka takrban mara mbili kwa usiku.
Mtu anapofanya safari nyindgi chooni usiku, hupata matatizo ya kulala, hali ambayo husababisha pia msongo na uchovu.
0 maoni :
Chapisha Maoni