Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

ASERNAL YASITISHA MAZUNGUMZO NA SANCHES NA OZIL

Arsene Wenger: Arsenal imesitisha mazungumzo na Sanchez na Ozil

 Sanchez and Ozil

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema klabu hiyo imesitisha kwa muda mazungumzo kuhusu mikataba ya Alexis Sanchez na Mesut Ozil hadi mwisho wa msimu.
Mshambuliaji wa Chile Sanchez na kiungo wa kati wa Ujerumani Ozil, wote wenye umri wa miaka 28, wamesalia na chini ya miaka miwili kwenye mikataba yao.
Wenger amesema tayari amefanya uamuzi wake kuhusu mustakabali wake Arsenal, lakini bado hajatia saini mkataba wa miaka miwili aliopewa na klabu hiyo.
"Kwa sasa hatujaafikiana," Wenger alisema kumhusu Sanchez.
Akiongea na BeIn Sports, Mfaransa huyo wa umri wa miaka 67 alisema:
"Tumeamua kuangazia mwisho wa msimu na tuandae mazungumzo majira ya joto.
"Hali ni sawa kwa Ozil, kwa sababu unapokosa kupata makubaliano na mashauriano bado yanaendelea, hilo si jambo jema.
"Ni vyema kuketi na kuiangazia majira ya joto."

 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni