Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

VIONGOZI 4 WA CUF WALIOKWENDA KUSHEREHEKEA KUAPISHWA KWA WENZAO 7 WAMEPATA AJALI NA KUFARIKI DUNIA

Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho.

=========

Viongozi wanne wa CUF wamefariki kwenye ajali wakitokea Dodoma
Capture.PNG 21272279_2075016789179395_8804382814031940104_n.jpg
Stori iliyonifikia asubuhi hii ya Jumatano September 6, 2017 ni kwamba Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani. Ajali iliyohusisha gari aina ya Noah na Lori katika eneo la Ubena barabara ya Morogoro Mkoani Pwani.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdallah Kambaya Viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja Uredi.

Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni hawazidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni