Unaweza kudhani najichanganya sasa kwa post zangu mwenyewe! La hasha kuna kitu tofauti kabisa kwenye hii mada
Nazungumzia wale wapendwa wetu walitwaliwa kutoka maisha haya lakini
unahisia za ukaribu kabisa kuwa hawako mbali nasi, na kuna wakati tukiwa
pekeyetu tunahisi kabisa tuko nao pamoja, ni experience ya ajabu na ni tofauti kabisa na ndoto za usiku
Inawezekana kabisa ni hallucinations lakini kwanini itokee kwa hawa
baadhi tu na si wengine wote? Je ni kweli wamekufa ama wapo hai kwa
namna nyingine? Kwakuwa zile hisia za uwepo wao huwa halisi kupita kawaida
Mara nyingi huwa ni wazazi ndugu watoto jamaa marafiki na hata majirani,
sometimes ni watu ambao wala hatukuwa na ukaribu nao lakini
tulifahamiana... Kifo kina siri nyingi na hii ni mmojawapo.... Wafu walio hai
Usuwaze kuwa kafaje, usiwaze ushirikina wala misukule, wengine hufa vifo
vya kawaida kabisa tena baada ya kuugua muda mrefu......
Maajabu ni mengi dhana ni nyingi kwenye hili lakini moja linaloweza kuwa
na hakika zaidi ni mawasiliano ya kiroho yaliyopo kati ya Wafu na walio
hai
Jihadhari usibebebwe na dhana potofu unapokumbana na hiyo hali kisha
ukawasimulia walimwengu watakaokuja na dhana za misukule! Ama kurogwa!
Jihadhari sana! Mawasiliano ya wafu na walio hai ni mengi na hutokea
kwa namna tofauti tofauti.... SUUi kila kitu ni uchawi ... Vingine ni
asili ambavyo ufahamu wa kibinadamu haujavipatia majibu yote.... Wafu
waishio ni mfano hai na halisi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni