Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MKUU WA WILAYA YA HAI ADAI KWANINI ASHTAKIWE MWENYEWE?

Huyu mkuu wa Wilaya ya Hai alienda kuharibu shamba la mbunge wa Hai Mhe. Mbowe tena aliliharibu kwa mbwembwe mbele ya Camera za Video, Sasa leo analalamika nini?
Jana mahakamani alikuwa akilalamika kwamba kwanini ashitakiwe peke yake?

  Baadhi ya watu waliuliza, alipoenda kuharibu shamba la Mbowe alienda na nani?

Alimshirikisha Mkuu wa Mkoa au Mwanasheria wa Serikali?

"Mnapenda sana sifa, ngoja muone matokeo ya Kukurupuka".
alisema mwananchi mmoja
aliendelea kusema "Mimi nlimuona Mkuu wa Wilaya kwenye picha akiharibu shamba la Mbowe tena aling'oa huku amesindikizwa na askari.
"
"Hii iwe fundisho".
alisisitiza
 Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ameiomba Mahakama imuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika kesi ya madai ya fidia ya Sh549 milioni iliyofunguliwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Kiini cha kesi hiyo ni hatua ya Byakanwa, kudaiwa kuharibu miundombinu ya umwagiliaji ya shamba (green house) la kampuni ya Kilimanjaro Veggie Ltd (KVL) linalomilikiwa na Mbowe, Juni 19.

Mbowe, ambaye ni mbunge wa Hai na mkurugenzi mwendeshaji wa KVL, amemshtaki mteule huyo wa Rais kama mtu binafsi.

Ombi la kutaka AG aunganishwe, liliwasilishwa mahakamani jana na wakili Modestus Njau anayemtetea Byakanwa mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Aishiel Sumari.
19105705_1782120875431463_3351093519499668137_n.jpg 19247902_1170228936415850_7634718870478757744_n.jpg 19105964_324039318025853_5703089896265032751_n.jpg 19961284_1791562094193756_450173877565650494_n.jpg
Hizi ni picha zinazomuonesha Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa akiharibu shamba la Freeman Mbowe


Chanzo: Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni