Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MJUE TYNDALE ALIYEUAWA KWA KUTAFSIRI BIBLIA KWA KIINGEREZA, LAKINI NA KAHABA ALIYETAJWA KWENYE BIBLIA UFUNUO 17

Mwanamke (yule Babeli) wa Ufunuo 17 anaelezwa kuwa
“alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, Siri [2 The. 2:7], Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba” [Ufu. 17:5, KJV].

Asema hivi yule Nabii:

“Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.” Babeli anatangazwa tena kuwa ni “mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.” Ufunuo 17:4-6,18.
[​IMG]
                           Tyndale aliuliwa na utawala wa kipapa kwa kutafsiri biblia...



Mamlaka ile iliyodumisha utawala wake wa kidikteta juu ya wafalme wa Ulimwengu ule wa Kikristo kwa karne nyingi ni Roma. Rangi ile ya zambarau na nyekundu, dhahabu na kito cha thamani, na lulu, huonyesha waziwazi picha ya utukufu wake na fahari yake iliyozidi ile ya kifalme [angalia pia rangi za sare za viongozi na mapambo yao],
[​IMG] [​IMG]
mambo ambayo jimbo lile la Roma ( Vatikani), lenye majivuno makuu, lilijigamba kuwa nayo. Wala hakuna mamlaka [serikali] nyingine ambayo kweli ingetangazwa kuwa ilikuwa imelewa kwa damu ya watakatifu,” kama ya kanisa lile ambalo kwa ukatili mbaya sana limewatesa wafuasi wake Kristo.

Babeli pia anashtakiwa kwa dhambi ya kuungana isivyo halali [kuzini] na “wafalme wa nchi.” Ilikuwa ni kwa njia ya kujitenga mbali na Bwana, na kuungana na washenzi [wapagani], ndipo kanisa lile la Kiyahudi likageuka na kuwa kahaba [Soma Ezekieli 23]; naye Roma [kama kanisa], akifanya uasherati [ukahaba] unaolandana kabisa na ule na kutafuta msaada [kuungwa mkono] toka kwa mamlaka [serikali] zile za kidunia, anapata lawama iyo hiyo.

[​IMG] [​IMG]
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni