Mamake Zari Hassan aaga dunia
Zari Hassan anaomboleza kifo cha mamake miezi miwili tu baada ya kumzika aliyekuwa mumewe Ivan Ssemwanga.
Kulingana
na gazeti la daily nation nchini Kenya. Mfanyibiashara huyo ambaye ni
mke wa msanii wa bongo Diamond Platinum alithibtisha kifo cha mamake
Halima Hassan ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 58 asubuhi ya
Jumatano.Gazeti hilo limesema kuwa mfanyibiashara huyo alithibitisha habari hiyo ya kifo kupitia mtandao wake akichapisha picha ya marehemu mamake na kutangaza habari hizo.
''Ni huzuni kubwa kwamba familia yangu inatangaza kifo cha mama
yetu mpendwa aliyefariki asubuhi ya leo .Mungu aiweke roho yake mahali
pema peponi, Mungu akusamehe madhambi yako yote na akuweka
peponi.Tutaendelea kukupenda sisi watoto wako'', aliandika.Kulingana
na gazeti la Daily Nation kifo cha mamake Zari kinajiri siku mbili tu
baada ya Zari kuchapisha picha akiwa amekalia kaburi la aliyekuwa Mumewe
Ivan akiomboleza.
Mamake Zari alilazwa katika hospitali ya Nakasero mjini Kampala mnamo mwezi Juni baada ya kupata mshtuko wa moyo.
Baadaye alitolewa lakini akalazwa tena wiki iliopita.
Mama Halima amewaacha watoto watano.
Mamake Zari alilazwa katika hospitali ya Nakasero mjini Kampala mnamo mwezi Juni baada ya kupata mshtuko wa moyo.
Baadaye alitolewa lakini akalazwa tena wiki iliopita.
Mama Halima amewaacha watoto watano.
0 maoni :
Chapisha Maoni