Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

DAH, NGELEJA ARUDISHA HELA YA ESCROW MILIONI 40.4

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja amerejesha rasmi Serikalini fedha alizozipokea kutoka kwa James Rugemalira mnamo tarehe 12/2/2014 katika mgao wa Escrow ambazo ni kiasi cha Shilingi Milioni 40.4 ili kukwepa kuendelea kuandamwa na kashfa hiyo.

mh-william-ngeleja-waziri-wa-nishati-na-madini-akihutubia-pic-by-baraka-baraka.jpg
Ngeleja amesema kuwa ''Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo'' Ngeleja.

'Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi.

Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW nimeamua kuchukua hatua.

Kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuna harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.

Nimerudisha fedha hizi ili kulinda maslahi ya nchi yangu na heshima ya chama changu, Serikali, wanasengerema, familia yangu na heshima yangu.

Nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha kiasi cha Milioni 40.4 serikalini.

1.jpg 2.jpg
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni