Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

TRUMP BAADA YA MAHAKAMA KUMWEKEA NGUMU AJA NA MASHARTI MAPYA WAHAMIAJI WA KIISLAM

Trump atoa masharti mapya ya usafiri kwa nchi 6 za Kiislamu


Rais Donald Trump wa Marekani ametoa masharti mapya

 
Utawala wa rais Trump umeweka masharti mapya ya maombi ya Visa kutoka kwa mataifa sita ya Kiislamu pamoja na wakimbizi wote, ambayo yanawataka kuwa na mtu wanaohusiana ama ushirikiano wa kibiashara na Marekani.
Hatua hiyo inayoyahusisha mataifa yalio na Waislamu kama vile Iran, Libya,Somalia,Sudan ,syria na Yemen imeangaziwa katika ujumbe uliotumwa katika balozi zote.
Masharti hayo mapya yalioanza kufanya kazi siku ya Alhamisi yanaelezea mahusiano ya kifamialia kama mzazi, mkeo ama mumeo,mtoto wa kiume ama wa kike.
Masharti hayo yanajiri baada ya mahakama kuu nchini Marekani kuidhinisha kwa muda agizo la rais Trump ambalo lilikosolewa kuwa marufuku kwa Waislamu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni