Leo katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki ktk ajali . Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa
Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni
itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa
kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole .
Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi
wa Chadema watapaswa kutokuongea , nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro
Mh Ole Nasha , nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili
muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais
hasingeweza kukubaliana na ujinga huu.
Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani , jina langu lilikuwepo kwenye ratiba
kwa ajili ya salamu za rambirambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa
kukabidhiwa itifaki, mambo yalibadilika na ilionekana dhahiri kuwa
sitakiwi kabisa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na msiba
huu mbaya. M/kiti Mbowe aliandika meseji kwenda kwa M/ Rais kukumbusha
umuhimu wa wenyeji kutoa salamu , Makamu wa Rais baada ya kupokea meseji
hiyo, alimwita Mkuu wa Mkoa , ndipo ilionekana kama kuna ushindani
unatokea kati yao , lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa
salamu kwa wapendwa wetu.
Wabunge wa CCM waliokuwepo ambao ni mawaziri wote waliweza kutoa pole ,huu ni ubaguzi uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa, nitaeleza madhara yamo kwenye hotuba yangu kesho , lakini nafikiri watoto wanafuata walichofundishwa na wazazi ,pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais. Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.
Nawashukuru wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha, Mungu awabariki sana. Msiogope , Mungu hadhiakiwi apandacho mtu ndicho avunacho
LEMA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni