Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

PEPO LA BUNGE LA KUMNG'OA PROFESA MUHONGO LAMFUATA SAKATA LA MCHANGA TENA


          Image result for profesa muhongo images
Rais wa Nchi hii Dr John Magufuli anapokea ripoti ya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini ambao husafirishwa nje ya nchi makontena kwa makontena. Ripoti hii itatoa dira na mwelekeo wa miongozo inayotakiwa kufuatwa na kufanyika kunusuru rasilimali zetu kwa maslahi ya watz.
FUATILIA UZI HUU KWA LIVE UPDATES PIA FUATILIA KUPITIA TBC1
------------

--Updates..

3: 30 Asubuhi: Shughuli imeanza kwa wasanii kutumbuiza wimbo wa uzalendo.

Sasa Katibu Mkuu Ikulu, Mheshimiwa Balozi Kijazi anazungumza kwa utangulizi huku akibainisha kuwa ripoti inayosomwa leo ni ya Kamati ya Kwanza iliyoundwa na Rais na kueleza kuwa ripoti ya 2 itafuata siku zijazo.

Baada ya utangulizi, anamkaribisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof Mruma ili asome ripoti kabla ya kuikabidhi kwa Rais Magufuli.

Prof Mruma: Kamati hii baada ya kuteuliwa, tulianza kwa kuandaa mpangokazi, kupitia mafaili yote ya usafirishaji, kutembelea maeneo yote yenye makontena ili kuyachunguza na kuweza kuchukua sampuli. Katika kuchukua sampuli tulifuata taratibu za kisayansi ili kufanya sampling na kufanya uchunguzi wa materials zote.
Matokeo ya Uchunguzi
- Jumla ya makontena 277 yalifanyiwa uchunguzi.

- Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya madini ya dhahabu, copper, chuma na mengine ndani ya makenikia(mchanga) yaliyobebwa kwenye makontena.

Taarifa kutoka kwa wazalishaji na wakala wa serikali (TMAA);
Dhahabu tani 1.2 = Bilioni 7.5bilioni
Silver gramu 202.7 - 351/tani (iliripotiwa nusu tu ya gramu zilizomo kwenye kila kontena)
Sulphur 16.7 - 50.8/tani (kwa tani zilizopatikana 2161 kwa makontena 277)= Bilioni1.4
Chuma 13.6 - 30.6/tani (kwa kontena 277) = Bilioni 2.3
Copper 17.6 - 23.3/tani (kwa kontena 277) = Bilioni 13.6

(Reserved space for more data)

THAMANI YA JUMLA
(reserved space for data)

- Kamati imebaini kuna upotevu mkubwa wa mapato ya serikali ktk ukokotoaji wa mirabaha.

- Bahati mbaya madini haya (sulphur na chuma) hayahusishwi ktk kukokotoa mirabaha. Ni Silver, Shaba na dhahabu pekee ndio yanayoripotiwa.

- Kuna madini mkakati(strategic metals) ambayo yanalingana na dhahabu, hayakuhusishwa pia japo yanahitajika sana duniani kwa sasa na yana thamani kubwa.

Yote yalikuwa na thamani ya bilioni 129.5=261.5
(Reserved space for more data)

Mhe Rais, hivyo ndivyo viwango na mapato tuliyopoteza.

Pamoja na kuchunguza makenikia, kamati ilichunguza pia shehena ya mbale za shaba (38.9g kiwango cha dhahabu)

Katika kufuatilia utendaji wa TMAA, Kamati ilibaini kuwa;
- Haifungi utepe wa kudhibiti makontena (ufungaji unafanywa wakati kusafirisha tu). Hii inatoa fursa ya watu kuchezea viwango. Tunapendekeza wakala wafunge utepe mwanz

- Uwezo wa scanner inayoangalia yaliyomo kwenye makenikia ndaniya kontena ni hafifu. Mfano tulijaribu kuficha vipande vya chuma, scanner haikuona. Hivyo mtu akiamua kuficha vitu kwenye makenikia haviwezi kubainika.

Mapendekezo ya Kamati
1. Isitishe usafirishaji wa mchanga mpaka mrabaha stahiki utakapolipwa serikali kwa kuzingatia thamani halisi ya makenikia.

2. Ujenzi wa *** unafanyika haraka ili makenikia hayo yasafirishwe ndani ya nchi ili madini yote yaweze kufahamika na kutozwa mrabaha sahihi.

3. Tepe za udhibiti zifungwe mara moja ili kuepuka udanganyifu unaoweza kufanyika wakati wa kuchukua sampuli.

4. TMAA ipime metali zote zilizomo kwenye makenikia ili kupata thamani halisi ya metali hizo (mrabaha).

5. Kutokana na kuwepo madini mbalimbali kwenye Mbale. TMAA ipime viwango vya metali zote muhimu ktk mbale zinazosafirishwa bila kujali kilichoandikwa kwa msafirishaji.

6.

7. Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wale wa wizara inayohusika.

8. Pamoja na vyombo vya uhakiki, serikali iweke mfumo wa kushtukiza ili kuepuka watendaji kufanya kazi kwa mazoea.

9. Serikali itumie wataalamu wa mionzi ili kufunga scanner zenye uwezo sahihi (kwa ajili ya makenikia na mizigo mingine).

Mhe Rais, nichukue fursa hii kukushukuru kwa kuwa na imani na sisi na kututeua kutekeleza jukumu hili muhimu ili kuepusha nchi kupata hasara. Ni imani yetu kuwa matokeo ya uchunguzi hii yatatoa msaada mkubwa kwa serikali.

Shukrani kwa vyombo vya ulinzi na usalama, Wakala wa Jeolojia (Maabara mkemia mkuu), TPA, TRA, TMAA, Vyuo vya UDSM na MUM(kwa kutoa wataalamu).

Kamati hii iko tayari kutoa ufafanuzi pale utakapohitajika. Asante.
----------------

Prof. Mruma amemaliza kusoma ripoti hiyo na sasa zoezi la kumkabidhi Rais linaendelea.

========
Magufuli: (Anatambulisha wote waliohudhuria kulingana na itifaki), Tulitumia vifaa vyote katika ulinzi lakini wapo waliojitokeza kutaka kuingilia uchunguzi huu na bahati nzuri majina yote tunayo, wapo wengine mnawajua wenyewe wakibwatuka wengine kwenye mitandao, wamepewa fedha.
Ndugu zangu tuko kwenye vita na vita ya uchumi ni mbaya sana, mabilioni ya fedha haya ambayo nchi yetu imepoteza, dhahabu tani tani 7.8 hadi 13.16 kwa kontena 277. Tani 15.5 ni malori mawili na land rover moja. Malori mawili ya tani 7 yanaleta tani 14, labda na pick up zote umezipaki pale na hio ni kwa makontena 277.

Kuna kamati inayotaka kujua makontena yanasafirishwa mangapi, haraka haraka ni makontena 250 na 300 kwa mwezi, kwa mwaka zaidi ya makontena 3600.

Ni kitu cha kuumiza mno na kwa hili watanzania wote tushikamane, hospitali watu wanakosa madawa, mashuka, shule watu wanakosa madawati, hela za treni mpaka tukope kumbe kuna hela zinamwagika hapa.

Nilimfukuza katibu mkuu wa nishati na madini alipoulizwa na kamati ya wabunge kiasi cha dhahabu kilichopo, ni aibu kwa mtu aliesomeshwa na watanzania such a stupid comment.

Bilioni 676 hadi trilioni 1.5 tunazazipoteza watanzania, madini mengine hawakujali hata kuyarekodi(Nipe ile document). Tunaweza tukaona kwa miaka kwa 17, tulipaswa kuwa donor country kwa vitu tulivyopewa na Mungu.

Hauwezi ukashangaa katika wizara hizi ndio nilichagua watu wazuri wa kuziendesha, kuna tume iliundwa miaka ya nyuma, walidanganya kuna smelter ziko nchi fulani, walipoenda wakaishia hotelini. Smelter sio tatizo kwenye ripoti, inaonyesha kampuni nyingi zinazoweza kuuza smelter, viongozi hawakuchukua juhudi za kununua smelter.

Sera ya taifa ya madini ya mwaka 2009 inasema haja ya kununua smelter, viongozi wa hizo wizara hawakufanya juhudi, kwanini TMAA wapime kidogo halafu wanakuja kuweka tu seal wakati hujui kilichowekwa ndani, kwanini?

Kwanini wasimamizi wasimamizi wa TMAA ambao ni wizara hawakushtukia? Kwanini bodi ya TMAA haiwakushtukia? Inawezekana nikajiuliza maswali mengi majibu yasipatikane. Inawezekana yakaletwa na tume nyingine, nilienda na wenzangu kuteta kidogo, Haiwezi kupita hivi hivi.

Ripoti hii ikipita hivi hivi tutakuwa watu wa ajabu sana, tutafanya kitu, tunasubiri ile ripoti nyingine.

  1. Mapendekezo yote ya tume nimeyakubali
  2. Bodi ya TMAA nimeivunja Rasmi
  3. Namsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TMAA na wafanyakazi waanze kuchunguzwa na vyombo vya dola
  4. Shughuli zote zinazohusu madini, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vianze kutumika sawasawa.
Wizara wameshindwa kusimamia TMAA, ujenzi wa Smelter pia imeshindwa kuweka utaratibu wa kufatili haya makinikia, mbona huwa wanaenda Ulaya? Kamishna madini anafanya nini? Waziri anafanya nini?
Vyombo viwachunguze watendaji wa wizara ya nishati na madini wanaoshughulikia madini.

Nampenda sana Prof Mhongo lakini pia ni rafiki yangu, lakini kwenye hili, ajifikirie, ajitathmini na bila kuchelewa nilitaka aachie madaraka.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni