Matokeo ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma yameibua mapya mengine
Hiyo inatokana na mwenyekiti wa CCM wilayani Chamwino, Charles Ulanga
kuhoji sababu za kutajwa katika orodha ya walioghushi vyeti vya kidato
cha nne wakati hajawahi kusoma elimu ya Sekondari
Sakata la Mwenyekiti huyo ni mwendelezo wa utata ulioibuka baada ya
ripoti ya matokeo ya uhakiki huo uliobaini wafanyakazi 9,932 wa Serikali
na taasisi zake kuwa na vyeti vya kughushi, kutumia kwa watu wengine au
cheti kimoja kutumiwa na zaidi ya mtu mmoja
Utata huo umeibuka mkoani Kigoma, ambako jina la mganga mkuu wa mkoa limetajwa, likionekana kutumiwa na mfanyakazi wa Hifadhi ya Gombe iliyoko Kigoma
Akizungumza na gazeti hili jana baada ya jina lake kuwa miongoni mwa
wenye vyeti feki, Ulanga, ambaye pia ni Mratibu wa Elimu wa Kata ya
Buigiri wilayani Chamwino mkoani Dodoma, alisema wakati wa uhakiki
alipeleka cheti cha darasa la saba na cha ualimu daraja la tatu 'A'.
"Nawashangaa wapi walipopata cheti cha kidato cha nne kwa sababu mimi nilipeleka vyeti viwili; cha darasa la saba na cha ualimu. Sasa hiki cha kidato cha nne walichokikuta feki sijui wamekitoa wapi?" alihoji Ulanga
Mwenyekiti huyo alisema baada ya kumaliza darasa la saba aliomba kujinga na masomo ya ualimu kama utaratibu ulivyokuwa ukitaka wakati huo
Alijiunga na Chuo cha Ualimu Bustani kilichopo wilayani Kondoa mwaka 1980 na kutunukiwa cheti daraja la tatu "B"
"Wakati ule ulikuwa unaomba kwenda darasa saba niliomba kwenda chuo cha ualimu nikakubaliwa nikaenda Bustani na nilipata cheti cha ualimu daraja la tatu "B", alisema Ulanga
Chanzo: Mwananchi
Home
/
Uncategories
/
MWENYEKITI WA CCM CHAMWINO ASHANGAA KUTAJWA VYETI FEKI WAKATI HAJASOMA SEKONADARI YOYOTE
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni