Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MEYA WA ARUSHA NA WAANDISHI WA HABARI WAKAMATWA SHULENI LUCKY VINCENT

Majengo ya Shule ya Lucky Vincent, walipokamatwa Meya na Waandishi wa habari wakati wanapeleka rambirambi zao za faraja kutokana na msiba mkubwa ulioipata hiyo shule,

pic+shule.png
Meya wa jiji la Arusha muda huu amekamatwa na polisi akiwa katika shule ya Lucky Vincent! Sababu haswa hazijulikani.
Meya wa Arusha,viongozi wa dini na waandishi wa habari wamekamatwa na polisi muda huu eneo la shule ya Lucky Vincent,walikoenda kutoa rambirambi!

=====

Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.

Chanzo: Mwananchi
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni