Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

JAMBAZI SUGU MWANAMKE KENYA AUAWA NA POLISI KWA RISASI

Mwanamke anayedaiwa kuwa ni Jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi

[​IMG]
Mwanamke huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na mapema Jumatano katika mtaa wa Kayole.

Gazeti la kibinafsi la Daily Nation linasema mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wanne wa kiume pale walipofumaniwa na polisi wakitekeleza wizi katika eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole

Anadaiwa kufyatulia risasi maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao wakauawa huku wenzao wakifanikiwa kutoroka.

Taarifa katika gazeti la Daily Nation inasema polisi waliwaandama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzao kupitia Whatsapp kwamba majambazi hao waliokuwa wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa.

Chanzo: BBC
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni