Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

WAHAMIAJI HARAMU WARUDI PORI LA KARAGWE KWA KASI NA KIBURI


Wimbi la wahamiaji haramu ambao huingia na kundi kubwa la mifugo wakitokea nchi jirani limerudi upya tena safari hii kwa kasi na kujiamini na kiburi .


Wahamiaji hawa itakumbukwa walifurushwa na aliyekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Jakaya Mrisho Kikwete .

Wiki iliyopita Serikali ya mkoa wa Kagera inayoongozwa na Maj Gen Kijuu ilitangaza kupitia mkuu wake wa wilaya kuingia porini kuwasaka wahamiaji hawa hatari wenye silaha kali na nzito,matokeo yalikuwa mazuri na walikuta makundi hayo kama taarifa za intelligence zilivoonyesha .

Serikali ya mkoa ilitoa onyo kuwa kabla ya mwisho wa mwezi wataanzisha operesheni kubwa ya kijeshi kuusafisha mapori ya misitu hii ya mipakani..Moja ya madhara ya wahamiaji hawa wenye malengo yaliyo nyuma ya pazia ni mpango haramu wa EXPANSIONISM ambao unajulikana wazi kwenye anga za kijasusi
Wenzetu hawa wanafadhili wananchi ...wengi wao wakiwa sio wananachi wa kawaida bali askari wao wastaafu na wapelelezi kuhamia maeneo ya mipakani ya nchi hasa Tanzania na Congo ...wakishafika huko hujipenyeza katika mpango huu haramu wa kujipanua ....wakiwa na lengo la kuhakikisha miaka 10 na kuendelea wakikaa bila kusumbuliwa wanakuwa wameshajijengea uhalali, na katika kipindi hicho wanakuwa wanapenyeza silaha ...na ikifikia kuwaondoa itakuwa ni kama vita ....hii ndio pia iliyogundulika wakati wa operesheni kimbunga ....kuna maeneo Mapambano ya kuwahamisha wahamiaji yaliambatano na wao kujibu mapigo kwa kutumia silaha nzito za kubeba begani ..RPG, LMG.. na nyingine ..

KATIKA Hali inayotia shaka inasadikika kuwa mpango mzuri wa Maj Gen Kijuu na wenzake ambao ni ma DC Aliotoka nao jeshini tayari umehujumiwa kwa amri kutoka juu .
Tunaomba wanaoipenda nchi hii wawe macho na wafuatilie kwa makini haya yanayoendelea ...tunahitaji katiba mpya itakavyovipa vyombo vyetu vya ujasuri na jeshi uwezo wa kudhibiti hali kwa usalama wa taifa letu ...ili hata tukitawaliwa na "mgeni" asiwe na uwezo wa kuvuruga safu ya vyombo vyetu kwa kupenyeza watu wanaoweza kuwa tishio kwa nchi ..ingekuwa hawa wateule wanapita bungeni basi sio rahisi mtu kubadili safu namna hii ambayo inaweza kudaka taarifa za operesheni na kuzifikisha kwa adui ambaye ana uwezo wa kuwasiliana na walio juu kuzuia

Hili sio suala dogo!!
Source : Jamii Forum
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni